Saratani mlango wa kizazi yatikisa Kanda ya Ziwa

Muktasari:
Mkurugenzi Msaidizi wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Youth Foundation (Tayoa), Elizabeth Ndakidemia alisema hayo jana alipozungumzia kampeni ya uhamasishaji jamii kupima maradhi yasiyoambukiza. Mikoa iliyohusika katika upimaji kwa kipindi hicho ni Mwanza, Simiyu, Geita, Mara, Tabora na Shinyanga.
Mwanza. Wanawake 11,354 kati ya 11,871 waliopimwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kati ya mwaka 2014 hadi sasa, wamegundulika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.
Mkurugenzi Msaidizi wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Youth Foundation (Tayoa), Elizabeth Ndakidemia alisema hayo jana alipozungumzia kampeni ya uhamasishaji jamii kupima maradhi yasiyoambukiza. Mikoa iliyohusika katika upimaji kwa kipindi hicho ni Mwanza, Simiyu, Geita, Mara, Tabora na Shinyanga.
Ndakidemia alisema sababu zinazochangia kuongezeka kwa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake kuwa ni uelewa mdogo wa wananchi kuhusu ugonjwa huo na namna ya kujipima, mila, desturi, utamaduni wa baadhi ya makabili na gharama kubwa ya matibabu.