Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa atoa kauli ubunge wa Ruangwa

Waziri Mkuu wa Tanzania na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa leo Jumatano, Julai 2, 2025 ametangaza rasmi kutokugombea tena ubunge wa Ruangwa baada ya kulitumikia jimbo hilo kwa miaka 15.

Akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa ya mkoa na Wilaya ya Ruangwa leo Jumatano, Julai 2, 2025, Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi kwa kumuunga mkono wakati wote ambao amekuwa mbunge wa jimbo hilo.

"Imefika wakati kwa mshikamano tulioujenga sasa ni wakati wa kutoa fursa kwa wana-Ruangwa wengine wapenda maendeleo waweze kuunganisha nguvu hizi ili kaulimbiu yetu ya Ruangwa kwa maendeleo inawezekana iweze kusonga mbele zaidi."

Aidha, ametoa wito wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya kuwapa ushirikiano wagombea wote wenye nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Kadhalika, Majaliwa amewasihi wana-Ruangwa kuendelea kushikamana na itakapofika siku ya uchaguzi waweze kuchagua wagombea wote watakaowakilisha chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huo. 

"Viongozi wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dk (Emmanuel) Nchimbi watakapokuja tujitokeze kwa wingi kwenye mikutano tusikilize sera, lakini siku ya kupiga kura tuwapigie kura nyingi za kutosha."

Aidha, amemshukuru Rais Samia, viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumuamini na kumpa fursa ya kuwatumikia wana Ruangwa.

Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge wa Ruangwa mwaka 2010 na amehudumu kwa kipindi cha miaka 15.