Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Chalamila: Waliofariki Kariakoo sababu sio kukosa hewa

Muktasari:

  • Watu 42 waliojeruhiwa katika jengo la ghorofa Kariakoo 35 kati yao wameruhusiwa kurudi nyumbani, baada ya kupewa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mpaka jana jumla ya watu waliofariki dunia kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo, ilikuwa ni wanne huku sababu ikiwa sio kukosa hewa.

Chalamila ameyasema hayo leo Jumapili Novemba 17, 2024 wakati shughuli za uokozi zikiendelea katika jengo hilo lililoporomoka jana Jumamosi Novemba16, 2024.

"Mpaka muda huu waliokufa kwa kukosa hewa hatuna taarifa hiyo na hii ni kwa taarifa ya papo kwa hapo,"amesema Chalamila.

Pia, amesema wanaendelea kuwasiliana na watu waliokwama chini ya jengo hilo na wamepelekewa gesi, maji na glucose huku wakiwaomba kuendelea kuwa wastahimilivu.

Aidha, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imetoa orodha ya majina 40 ya manusura wa ajali ya jengo la ghorofa kuporomoka Kariakoo waliopelekwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, imesema hadi ilipotimu saa 11 jioni jana, manusura 35 waliruhusiwa kurudi nyumbani.


Idadi ya vifo

Mrakibu Mwandamizi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Peter Mtui, amesema hadi sasa (jana jioni) watu watano wamepoteza maisha huku wengine 42 wakijeruhiwa.

Shughuli ya kufukua kifusi inaendelea katika jengo hilo la ghorofa nne lililoporomoka asubuhi ya Jumamosi Novemba 16, 2024 katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Endelea kufuatilia Mwananchi...