Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa zamani Korea Kusini afungwa miaka 24 jela

Muktasari:

Mahakama ambayo imekuwa ikisikiliza shauri lake imemtia hatiani Ijumaa. Amepigwa faini pia ya dola za Marekani 16 milioni.


Seoul, Korea Kusini. Rais aliyeondolewa madarakani, Park Geun-hye amehukumiwa kifungo cha miaka 24 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa kadhaa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Mahakama ambayo imekuwa ikisikiliza shauri lake imemtia hatiani Ijumaa. Amepigwa faini pia ya dola za Marekani 16 milioni.

Wakati wa mchakato wa kesi hiyo, ilielezwa kwamba mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 66, alikula njama na rafiki yake Choi Soon-sil pamoja na msaidizi wa zamani wa rais kulazimisha makampuni makubwa kutoa mchango wa fedha katika mfuko ulioanzishwa kwa ajili ya kusaidia sera zake.

Alishtakiwa pia kwa kosa la kuomba rushwa kutoka kwa mkuu wa kampuni mama ya Samsung Group ili iweze kupewa upendeleo.

Hata hivyo, hakupatikana na makosa katika mashtaka mawili likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka kuhusu kuilazimisha kampuni ya magari ya Hyundai kufadhili tangazo la kampuni inayomilikiwa na Choi.

Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap limeripoti kwamba Park hakufika mahakamani kusikiliza hukumu ya kesi hiyo.

Amekuwa jela kwa muda wa zaidi yam waka mmoja, lakini amekataa kufika mahakamani karibu wakati wote kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa.

Park aliondolewa kwa kauli moja Desemba 2016 baada ya wabunge kupiga kura kumkataa bungeni lakini alikataa kujiuzulu, badala yake aliamua kuomba radhi huku akikana kosa. Miezi mitatu baadaye, jopo la majaji wanane wa Mahakama ya Katiba walipiga kura kwa kauli moja kumwondoa ikulu. Alishtakiwa rasmi, akakamatwa na kufukuzwa ofisini.

Mwanamama huyo ni binti wa Park Chung-hee, rais wa zamani aliyeshika madaraka 1961 na akauawa miaka minane baadaye.