Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkurugenzi wa Jatu aomba kuiachia mahakama kesi yake

Muktasari:

  • Gasaya anayekabiliwa na mashtaka mawili kikimo la kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu, kumwandikia barua DPP ya kuomba kukiri mashtaka.

Dar es Salaam. Peter Gasaya (33), mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Jatu PLC anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, amesema anaiachia Mahakama ishughulikie kesi yake.

Gasaya anakabiliwa na mashtaka mawili –kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha kiasi hicho cha fedha, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Kupitia wakili wake, Nafikile Mwamboma, mshtakiwa huyo ametoa ombi hilo baada ya upande wa mashtaka kueieleza Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi haujakamilika.

“Sisi upande wa utetezi, tunaiachia Mahakama itoe uamuzi wake, kwa sababu kila tarehe ya kesi hii inapotajwa upande wa mashtaka unakuja na jibu hilohilo kuwa upelelezi haujakamilika,” amesema Wakili Mwamboma.

Awali, Wakili wa Serikali, Cathbert Mbiling’i alidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa kutajwa na upelelezi wake bado unaendelea.

Mbiling'i ametoa maelezo hayo, leo Mei 9, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geofrey Mhini, anayesikiliza kesi hiyo.

Pamoja na hoja hizo, Hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 22, 2025 kwa ajili ya kutajwa na kuwa mshtakiwa ataendelea kubaki rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili halina dhamana.

Gasaya alifikishwa katika mahakamani hapo Desemba 29, 2022 na kusomewa kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa kati ya Januari mosi 2020 na Desemba 31, 2021 katika jiji la Dar es Salaam, akiwa kama mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, kwa njia ya udanganyifu alijipatia Sh5,139,865,733 kutoka Saccos ya Jatu.

Shtaka la pili ni kutakatisha fedha tukio analodaiwa kulitenda kati ya Januari mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika jiji la Dar es salaam kwa kujihusisha na muamala wa Sh5, 139, 865,733.

Anadaiwa alihamisha fedha hizo kutoka katika akaunti ya Jatu Saccos iliyopo benki ya NMB tawi la Temeke kwenda katika akaunti ya JATU PLC liyopo katika benki ya NMB tawi la Temeke, wakati akijua fedha hizo zinatokana na kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.