Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia: Tuendelee kuwa watulivu wakati uokoaji ukiendelea

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na taarifa ya ajali ya ndege ya shirika la Precision Air huku akiwataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu wakati uokoaji ukiendelea kufanyika.

Dar es Salaam. Saa chache baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Precision kupata ajali katika Ziwa Victoria, Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na tukio hilo.


Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Novemba 6, 2022 wakati ndege hiyo yenye namba PW 494 ilipokaribia kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia, ameandika: “Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya ndege ya shirika la Precision Air katika Ziwa Victoria, mkoani Kagera.


“Natuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii. Tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukiomba Mwenyezi Mungu atusaidie,” ameandika Rais Samia katika salamu zake hizo.


Wakati huohuo, Shirika la Ndege la Precision Air, limethibitisha ajali hiyo iliyohusisha ndege yake yenye namba za usajili PW 494.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 6, 2022 na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa shirika hilo, Hillary Mremi, ndege hiyo imepata ajali ilipokuwa inakaribia Uwanja wa Ndege wa Bukoba ikitokea Dar es Salaam.


“Timu ya uokoaji imetumwa eneo la tulio na taarifa zaidi zitatolewa baada ya saa mbili,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Ingawa inaelezwa ndege hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 43 kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila taarifa ya Precision Air haikuweka wazi idadi ya abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo.


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi za tukio hilo.