Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia awasili Usangi kuongoza mazishi ya Msuya

Muktasari:

  • Msuya alifariki dunia Mei 7, 2025 kwa ugonjwa wa moyo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mwanga. Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Usangi Kivindu kushiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya.

Msuya ambaye alizaliwa mwaka 1931 katika Kijiji cha Chomvu, Usangi, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro alifariki dunia Mei 7, 2025 kwa ugonjwa wa moyo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo Mei 13, 2025 katika makaburi ya familia yaliyopo nyumbani kwake.

Viongozi wengine ambao wameungana na Rais Samia katika msiba huo ni Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, Makamu wa Rais Dk Philip Mpango, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne,  Jakaya Kikwete.

Wengine ni  Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi, makatibu wakuu viongozi, mawaziri mbalimbali, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura,  pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye.

Ibada hiyo ya mazishi ambayo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini wakiwemo maaskofu inaongozwa na Mkuu wa KKKT, Dk Alex Malasusa.

Jana Mei 12, baada ya mwili wa kiongozi huyo kufikishwa katika viwanja CD Msuya, vilivyopo Wilaya ya Mwanga, walipata fursa ya kuaga mwili huo huku baadhi ya viongozi wa dini na Serikali wakitoa salamu za rambirambi.

Baada ya kumalizika shughuli ya kuaga mwili katika viwanja vya CD Msuya, msafara wenye mwili uliondoka uwanjani hapo kuelekea Usangi katika shule ya Sekondari ya Kilaweni, Usangi ambapo salamu mbalimbali za rambirambi nazo zitatolewa na wananchi wa eneo hilo walipata fursa ya kuaga mwili kisha mwili kupelekwa nyumbani.


Endelea kufuatilia Mwananchi taarifa zaidi.