Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia awasili Kenya kuhudhuria uapisho wa Ruto

Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya, William Ruto leo Jumanne Septemba 13, 2022. Picha na Ikulu

Muktasari:

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Kenya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais mteule wa Kenya, William Ruto.

Nairobi. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Kenya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais mteule wa Kenya, William Ruto.

Raisa Samia ambaye tayari ameshawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi atakuwa miongoni mwa wakuu wa nchi na wageni mbalimbali watakaoshuhudia Ruto akiapishwa kuwa Rais wa Kenya leo Jumanne, Septemba 13, 2022 katika Uwanja wa Kasarani.

Ruto anaapishwa leo kuchukua nafasi ya Uhuru Kenyatta, ambaye anamaliza muda wake wa utawala wa miaka kumi aliyoianza Aprili 9, 2013, akivaa viatu vya Mwai Kibaki.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa jana Jumatatu ilisema, Rais Samia ataambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wa Tanzania na Zanzibar, akiwemo Balozi Libarata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje.

Ruto ambaye ni Naibu wa Rais, ataanza safari ya kuwaongoza Wakenya, baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022 kwa kumshindi hasimu wake wa karibu, Raila Odinga mwenye miaka 77.

Mbali na Ruto mwenye miaka 55, mwingine atakayeapishwa leo ni Naibu wake wa Rais, Rigathi Gachagua.

Rais huyo mteule wa Muungano wa Kenya Kwanza, alipata kura milioni 7.1 sawa na asilimia 50.49 huku Raila wa Muungano wa Azimio akiambulia kura milioni 6.9 sawa na asilimia 48.8

Baada ya matokeo hayo, Raila aliyekuwa akiungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta alipinga matokeo hayo katika Mahakama ya Juu nchini humo ambayo ilisikiliza kesi hiyo na kuyatupilia mbali mapingamizi aliyokuwa ameyaweka dhidi ya Ruto.

Katika uamuzi wake, Jaji Mkuu Martha Koome alisema Raila na waleta maombi wenzake walishindwa kuthibitisha kulikuwa na udanganyifu na uchakachuaji wakati wa mchakato wa kuelekea uchaguzi, siku na baada ya kupiga kura.

Baada ya kiapo hicho, Kenyatta atakuwa ni Rais mstaafu. Marais wengine waliowahi kuongoza taifa hilo ni, Jomo Kenyatta, Daniel Moi na Mwai Kibaki ambao wote wamekwisha fariki kwa nyakati tofauti.