Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Profesa Kabudi ataja matokeo tarajiwa Daraja la JP Magufuli

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Kabudi, nchi itakavyoweza kujenga barabara kwenda kutuunganisha na Afrika ya Kati inayopakana na Uganda, Congo Brrazavile na nchi za Afrika Magharibi, miaka 15 ijayo daraja hilo litakuwa kiungo kwa nchi za Afrika ya Kati na Magharibi.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema daraja la JP Magufuli linakwenda kuimarisha diplomasia ya kiuchumi na kindugu pamoja na kuendeleza sifa ya Tanzania kuwa lango la nchi nyingine za Afrika Mashariki na kati.

Amesema katika diplomasia, daraja hilo linaloongoza kwa urefu Afrika Mashariki ni kiungo katika kukuza uchumi wa mataifa yanayopakana na Tanzania.

Kabudi ameyasema hayo jana Jumapili Juni 22, 2025 kwenye Kongamano la Jukwaa la Fikra lililoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, linalojadili mada isemayo, ‘Kujenga Madaraja, Kujenga Taifa, Miundombinu kama Kichocheo cha Ukuaji Jumuishi’.

Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza kuhusiana mada kujenga madaraja, kujenga Taifa wakati wa Mwananchi Jukwaa la Fikra linalofanyika jijini Dar es Salaam leo.Picha  na Michael Matemanga

Akielezea ni kwa kiasi gani miradi mikubwa kama daraja hilo la Kigongo Busisi linaunganisha watu, nchi na kuleta tija katika uchumi, Profesa Kabudi alielezea matokeo chanya yatokanayo na ujenzi huo, akianza kuelezea historia ya diplomasia ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Rais Samia ni mwanadilomasia mahiri, tujikumbushe amekuwa sehemu ya diplomasia akiwa Waziri Zanzibar hasa baada ya kukua na mikutano ya kisiasa Zanzibar na kulazimika ujumbe wa Tanzania kutembelea mataifa mbalimbai duniani kueleza hali ya Tanzania na Zanzibar,” amesema.

Amesema baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 alienda yeye na Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete, lakini wakati huo aliyekuwa Waziri Zanzibar, baadaye makamu wa Rais na baadaye Rais Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Amesema katika kipindi chake akiwa Makamu wa Rais alifanya kazi kubwa za kidiplomasia hasa katika nchi za kusini mwa Afrika na kwingineko na baada ya kuwa Rais amekuza na kuendeleza demokrasia katka nchi za Afriksa Mashariki, Jumuiya ya Afrika na kusini mwa Afrika na duniani kwa ujumla.

“Sasa ili tuweze kujua umuhimu wa daraja hili, hatuna budi kujua jiografia ya Tanzania na Dk Samia ameitumia jiografia hii vizuri sana,” amesema.

Amesema Tanzania ndiyo yenye ukanda mrefu wa bahari na hivyo kuwa na bandari nyingi kuliko nchi nyingine yoyote na hata mpaka wa Mlima Kilimanjaro unapinda kwenda baharini lengo lilikuwa kuwawezesha Waingereza kuwa na bandari ya Mombasa na kwamba toka mwanzo Mlima Kilimanjaro ulikuwa eneo la Wajerumani.

“Kwahiyo ukiuliza kwanini Kilimanjaro ipo Tanzania sababu Mombasa ipo Kenya ilikuwa kuwapa bandari, kwahiyo sisi tuna jiografia inatuunganisha na nchi zingine zote na sisi tu ndiyo nchi yenye majirani wengi kuliko nyingine ya Afrika Mashariki tunao Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, DRC, Msumbiji, Zambia na Malawi.

“Sisi ndiyo lango la kwenda nchi zote hizo, kabla ya ujenzi wa barabara na reli bado Zanzibar na Bagamoyo ndiyo ilikuwa lango kubwa la kwenda huko, leo ni daraja letu kwahiyo daraja la Magufuli, Rais Samia alilikuta likiwa asilimia 25 leo amelikamilisha,” amesema.

Profesa Kabudi amesema daraja hilo limetuwezesha kujenga uwezo wa kuendelea kuzihudumia nchi zote hizo na wengi wanazungumzia mikoa wa kanda ya ziwa, yeye anauingiza Mkoa wa Kigoma kwani pamoja na barabara ya kwenda huko inaunganisha maeneo mengi.

Ikiunganisha Kahama kwenda Lunzewe lakini bado unaweza kwenda na daraja hilohilo mpaka Lunzewe, Kibondo, Kasulu, Kigoma, Buhigwe, Manyovu na Burundi, hivyo katika majadiliano ya daraja hilo siyo tu Geita, Mwanza, Kagera lakini pia mkoa wa Kigoma.

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, daraja hilo ni muhimu kwa sababu Rais ameimarisha sana utengamano wa kiuchumi katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Tunazungumzia uhuru wa aina nne, uhuru wa watu kwenda kufanya kazi, kusafirisha mizigo na uhuru wa huduma. Hamuwezi kuwa na uhuru wa watu kutembea na bidhaa bila kuwa na miundombinu,” amesema,

Ametaja daraja hilo linakwenda kuimarisha diplomasia ya kiuchumi ambayo ni moja ya mambo ambayo Rais Samia ameyasimamia kwa kiasi kikubwa, linajenga diplomasia ya uchumi lakini piav imekwenda kuimarisha diplomasia ya udugu kwa sababu watu wote tunafanana na kushabihiana.

“Daraja hili miaka ijayo tutakavyoweza kujenga barabara kwenda kutuuunganisha na Afrika ya Kati inayopakana na Uganda kwenda kutuunganisha na Congo Brazavile, na nchi za Afrika Magharibi miaka 15 ijayo itakuwa kiungo pia na nchi za Afrika ya Kati na magharibi,” amesema.

Profesa Kabudi amesema daraja hilo litafanya Tanzania ihitaji kuwa na bandari nyingi zaidi.

Katika hatua nyingine, Kabudi amesimulia namna Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM, kilivyojengwa kwa fedha za Watanzania akihusisha na ujenzi wa daraja la JP Magufuli.

Kabudi amesema wakati tunajadili ujenzi wa daraja la JP Magufuli kwa kutumia fedha zetu wenyewe, Chuo Kikuu chote cha Dar es Salaam tumekijenga wenyewe tofauti na nchi za Kenya na Uganda.


Amesema wakati nchi inapata uhuru mwaka 1961 kwa sababu za kihistoria, kisheria Tanganyika haikuwa koloni la Uingereza, bali ilikuwa nchi ya udhamini wa umoja wa mataifa chini ya utawala wa Uingereza  kama ambavyo Rwanda na Burundi ilikuwa chini ya udhamini wa umoja wa mataifa ikiwa chini ya utawala wa Wabelgiji na makoloni mengine kama Togo na Namibia.

Amesema nchi iliachwa nyuma kimaendeleo, hivyo inapata uhuru mwaka 1961 Mwalimu Nyerere alikuwa Waziri Mkuu, Mei Mosi, 1961 na uamuzi wake wa kwanza ilikuwa  ni kujenga chuo kikuu na kilianza bila jengo na wanafunzi 14 wa sheria na katika hao mmoja alikuwa mwanamke na walimu watatu.

“Msichana yule mmoja ambaye yu ngali hai, aliishi hosteli na kilivyoanza makao makuu yake ni ilikuwa jengo la Tanu ambalo leo ni CCM Lumumba, Mwalimu akalitoa jengo hilo lianzishe tumehamia UDSM  mwaka 1964 moyo wa kujenga hayo mambo ndiyo msingi na chuo hiki ndiyo kimekuwa chuo mashuhuri bara la Afrika kwa uleta wasomi kutoka nchi mbalimbali,” amesema Kabudi.

Akichangia mada hiyo, Balozi John Ulanga amesema asilimia 30 hadi 50 ya bei ya bidhaa ni gharama za usafirishaji hivyo maboresho yanapofanywa katika miundombinu yanapunguza gharama za usafiri kuongeza faida.

Amesema Tanzania ni eneo la kumkakati na nchi pekee iliyofungamana na nchi nyingi hivyo maboresho kama hayo yanayoondoa usumbufu wa mtu kusubiri kivuko, mara kivuko kimeharibika au sababu nyingine zinazokwamisha utendaji wa kivuko.

“Ujenzi huu unaonheza ufanisi, unaondoa usumbufu wa watu kufanya biashara kwani kitu ambacho wafanyabiashara wanaangalia ili kufanya biashara na nchi ni uhakika wa usafiri, natokaje nafikaje. Huu ni ufanisi mkubwa katika eneo la ushoroba wa kati na inaongeza ushindani ndani ya Afrika ya Mashariki,” amesema.