Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jokate ‘awamegea’ siri vijana kutoboa kipindi cha Rais Samia

Muktasari:

  • Asema vijana wakishikamana, kushirikiana na kuwa na mawazo chanya, wataweza kutumia fursa zilizopo kwa kushiriki kwenye miradi ya kimkakati ya Taifa na kuonyesha ushiriki wao moja kwa moja.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo amewataka vijana kujipanga na kushikamana ili kutumia fursa zilizopo, huku akisema unahitajika mpango wa Kitaifa kuwawezesha katika muktadha wa kifedha na ushirikishwaji kwenye miradi ili waonyeshe ushiriki wao moja kwa moja.

Amebainisha kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ili wahesabike kwenye meza za maamuzi, kuna mambo wanayotakiwa wayazingatie ikiwa ni pamoja na kujiendeleza kielimu, kuwa na mawazo chanya na kushirikiana.

Jokate ameyasema hayo jana Juni 22, 2025 kwenye Kongamano la Jukwaa la Fikra lililoandaliwa na Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, linalojadili mada isemayo, “Kujenga madaraja, kujenga taifa, miundombinu kama kichocheo cha ukuaji jumuishi”.

“Nchi hii tangu kuundwa kwake iliundwa na vijana, nafasi ya vijana kwenye ujenzi wa nchi imekuwa mwendelezo sisi kama vijana wa leo tunatakiwa tuwe mbele tukae kwenye meza za maamuzi, hata mwaka huu tuna Uchaguzi Mkuu sisi kama jumuiya tumekuwa sehemu ya kuhamasisha vijana wasiwe sehemu ya kulalamika,” amesema.

Amesema ili wahesabike kwenye meza za maamuzi, kuna mambo wanayotakiwa wayazingatie ikiwa ni pamoja na kujiendeleza kielimu, kuwa na mawazo chanya na kushirikiana na wenzao.

Jokate amesema katika midahalo mbalimbali wanayoifanya, wamekuwa wakiangalia namna gani vijana wanakuwa na tija kwenye Taifa lao.

“Kama nitakiuka Itifaki, lakini niseme tu vijana 800,000 sawa na asilimia 80 walitoa maoni wakati wa uandaaji wa dira ya mwelekeo wao, hata kwenye ilani yetu tuna vijana waliojitolea kupita nchi nzima na kuja na maoni.

“Kati ya mapendekezo ni pamoja na kuwa na nyumba nafuu kwa ajili ya vijana na Rais Samia ameyapokea maoni hayo kutoka kwa vijana wenyewe na imeingizwa kwenye ilani, inakwenda kufanyiwa kazi,” amesema Jokate.

Amesema tafiti ya nguvu kazi ya Taifa, vijana wana asilimia 55 na kwamba katika wanufaika na wawezeshaji wa hiyo miradi ni vijana, kwahiyo nafasi ya vijana haiwezi kuwa ndogo.

Akizungumzia kuhusu uongozi kwa vitendo, Jokate amesema shabaha ya Rais Samia ni kuona Tanzania inasonga mbele, na hiyo ndiyo sababu aliamua kumalizia miradi yote aliyoikuta bila kujalisha nani ameinzisha, mradi utaitwa jina jingine lakini yeye amesimamia mpaka kukamilika kwake.

“Kwahiyo kwangu mimi yeye ni kielelezo cha na tafsiri inayoishi ya neno kiongozi, sisi kama vijana tusiwe wabinafsi, tusijijali wenyewe, tuangalie maslahi mapana ya Taifa letu kama alivyofanya na anavyoendelea kufanya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Na ndiyo maana sisi kama vijana tunasema tusipotoboa kipindi cha Rais Samia, tusiposhikana mikono ili tufanikiwe katika kipindi chake ambacho ameweka maslahi mapana ya nchi sijui…sijui... Tutumie fursa ya kuwa na Rais kama huyu, tushikamane vijana tuweke vipaumbele vyetu vizuri na tujue Rais ni mama msikivu, mwelewa, yupo tayari kuona anatuvusha kama Taifa hususani sisi kundi la vijana,” amesema Jokate.

Alipozungumzia kuhusu nafasi kwa vijana katika miradi mikubwa nchini, katika muktadha wa kiuchumi na kijamii amesema unahitajika mpango wa kitaifa kuwezesha vijana katika ushiriki ujenzi wa miundombinu kwa kuwashirikisha katika miradi mbalimbali.

Amesema vijana wanapaswa kuwezeshwa kwenye miradi katika muktadha wa kifedha na ushirikishwaji kwenye miradi hiyo ili waonyeshe ushiriki wao moja kwa moja.

Akizungumzia mradi wa Daraja la la JP Magufuli amesema ujenzi wa mradi kama huo ni fursa na vilevile matumizi ya teknolojia lakini pia na zabuni ambazo zinanufaisha vijana nchini.

Amesema daraja hilo limetoa ajira hasa za wazawa vijana huku ikiwa ni fursa za ajira kwao kwa muda mrefu na mfupi. Akieleza zaidi amesema ni fursa kwa vijana huku akisisitiza wanapaswa kuacha kulalamika bali kufuata fursa zilipo.

“Ukiangalia kwenye hili daraja lililozinduliwa Waziri ametuambia kulikuwa na ajira 35,000 kati ya zile 32,000 wazawa sawa na asilimia 92 ukichunguza wengi walioshiriki ni vijana, hivyo ni fursa kwa vijana kwa ajira za muda mfupi na mrefu,” amesema.

Jokate amesema baada ya daraja kukamilika halihusiani na usafirishaji au kusafiri bali ni fursa ya kuongeza masoko ya kibashara, mambo hayo kwa kiasi kikubwa yanafanywa na vijana.

Amesema kuna fusra za kidijitali na ubunifu, miradi kama hiyo inapokuja huwapa vijana maono makubwa, kuona daraja kama hili limetekelezwa akili zao zinaanza kupanuka na kuona kwamba na wao namna gani wanaweza kubuni miradi mbalimbali.

Lakini amesema madaraja kama hayo hayawezi kufanikiwa bila kutumia teknolojia za kisasa, kwahiyo waliopo katika mifumo ya kidijitali wanapata fursa ya kuonyesha uwezo wao.

“Kwenye masuala ya zabuni na mafunzo, vijana wamenufaika kwa namna moja ama nyingine na waziri akitoa takwimu anaeleza namna gani vijana wamepewa mafunzo na kushiriki miradi ya kimkakati na sehemu ya biashara,” amesema.


Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Hannibal Bwire amesema daraja la Kigongo -Busisi ni kiungo muhimu katika njia za usafirishaji za ushoroba wa kati nchini.

Pia, amesema daraja hilo limebuniwa ili kuchochea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ya taifa kwa ujumla.

"Barabara zinapoboreshwa katika maeneo kama haya, thamani ya ardhi huwa inapanda.

"Moja ya athari ni kuongezeka kwa magari yanayopita kwenye daraja hilo, jambo linalofanya kuwapo kwa umuhimu wa kufanya tathmini na udhibiti wa kina katika maeneo ya kuingilia," amesema Bwire.