Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwigulu ataka magereza kulima chakula cha kutosha

Muktasari:

Akizungumza na viongozi wakuu wa mkoa toka uhamiaji, polisi, zimamoto pamoja na magereza leo kwenye ukumbi wa ofisi za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake  Mwigulu alimtaka mkuu wa gereza mkoa kuhakikisha analima mazao yatakayo tosha kulisha wafungwa, vyuo pamoja shule za sekondari na hivyo kuweza kuipunguzia Serikali gharama za kulisha .

Ruvuma. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameuagiza uongozi wa magereza Mkoa wa Ruvuma kuwatumia wafungwa waliopo kuzalisha chakula kwa wingi ili kuipunguzia gharama Serikali.

Akizungumza na viongozi wakuu wa mkoa toka uhamiaji, polisi, zimamoto pamoja na magereza leo kwenye ukumbi wa ofisi za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake  Mwigulu alimtaka mkuu wa gereza mkoa kuhakikisha analima mazao yatakayo tosha kulisha wafungwa, vyuo pamoja shule za sekondari na hivyo kuweza kuipunguzia Serikali gharama za kulisha .

Vilevile, amemuagiza  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk Bilinith Mahenge kuwasaidia magereza ekari 10,000 nyingine ili zianze kuandaliwa kuanzia sasa hadi kufikia mwezi Julai ziwe tayari kwa ajili ya kilimo hivyo kuongeza uzalishaji wa chakula msimu ujao ambapo bajeti iliyopo iweze kusaidia kununua  vifaa vya kilimo .