Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua zaendelea kuwa kilio kwa wakazi wa Dar

Muktasari:

  • Wamiliki wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu walia changamoto ya usafiri kutokana na maji kuendelea kujaa maeneo sugu ambayo kwa muda mrefu yamekuwa na changamoto hiyo kila mvua zinaponyesha.

Dar es Salaam. Bado mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam zimeendelea kuwa kilio kwa wakazi wake kutokana na adha ya usafiri wanayoipata kufuatia baadhi ya barabara kujaa maji.

 Hayo  yanathibishwa na baadhi  ya wamiliki wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu wanaodai maeneo mengi yaliyokuwa sugu kwa kujaa maji kipindi cha mvua kama Jangwani na Kamata yameendelea na hali hiyo  jambo linaloleta kero kwao.

Mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia alfajiri ya kuamkia leo Juni 5, 2023 zimeleta madhara mbalimbali kwa wakazi wa jiji hili ikiwemo kushindwa kufika kazini kwa wakati.

Wakizungumzia changamoto hizo watumiaji wa barabara jijini hapa wamedai licha ya kujengwa kwa lami zimekuwa zikijaa maji kiasi kwamba hata watumiaji wa vyombo vya usafiri wanaogopa kupita.

“Eneo la Kamata limekuwa sugu limekuwa likitusababishia vyombo vyetu kama hizi pikipiki kuharibika,’’ amesema Joseph Stanley ambaye ni dereva wa bodaboda eneo la Kamata.

Hoja hiyo imeungwa mkono na Charles Amos ambaye ni mkazi wa Kariakoo amesema afya zao zinakuwa hatarini kwasababu wanatembea kwenye barabara ambazo zimejaa maji ambayo hawajui yanatoka wapi.

“Kwa mfano hapa Kariakoo kuna watu wanazibua vyoo na kuviacha vitiririshe uchafu. Kwa sisi watembea kwa miguu tunapita katika maji haya tunakuwa hatarini kupata magonjwa kama fangasi,”amesema Amos

Issa Juma dereva wa daladala ameiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia katika maeneo ambayo yamekuwa kero kipindi cha mvua kwani magari yao yanakuwa hatarini kuharibika.

“Maji yakijaa hadi kiwango fulani inakuwa shida kupitisha magari kwani yanaingia ndani ndiyo maana mnaona tunalazimika kupita maeneo mengine kuhofia kuipita sehemu zenye maji mengi kulinda vyombo vyetu,”amesema

Amesema barabara nyingi zimekuwa na mshimo makubwa na unakuta sehemu hiyo maji yamejaa hivyo inakuwa vigumu kupata ramani nzuri ya kupita na kujikuta imeingia kwenye shimo.