Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muhimbili kupoteza Sh16.73 bilioni kwa kukopesha bila mkataba

Muktasari:

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) itapoteza Sh16.73 bilioni baada ya kutoa huduma bila mkataba kwa wateja wake, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini.


Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) itapoteza Sh16.73 bilioni baada ya kutoa huduma bila mkataba kwa wateja wake, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini.

Mkopo wa kwanza ulioainishwa kwenye ripoti hiyo, MNH iliwapatia huduma ya mkopo wa Sh3.63 bilioni wateja wake wanne bila mkataba.

Pia, ripoti hyo ya mwaka 2021/2022 ilibaini, wateja wawili katika hospitali hiyo walikuwa na mikataba iliyoisha muda kwa zaidi ya siku 122.

Muda huo ni kuanzia siku ya kuisha kwa mkataba hadi Juni 30, 2022 ambapo huduma zilizotolewa kwa wateja hao wawili zina jumla ya Sh13.10 bilioni.

Akizungumzia dosari hiyo kisheri, Wakili Joseph Kidumbuyo wa Kampuni ya Mawakili ya Firm ni Caden Dante Attorney ya mkoani Kilimanjaro, amesema kilichofanywa na MNH ni kosa kwani taasisi yoyote ya umma inafanya mawasiliano kwa njia iliyorasmi ya maandishi.

“Huyo aliyekopeshwa alikopeshwa kwa utaratibu upi? nani alihidhinisha mkopo wake, yapi masharti ya kulipa mkopo huo, je mkopo huo una dhamana? kama una dhamana, je dhamana hiyo ni ipi na imewekwa kwa utaratibu upi,” alihoji wakili huyo.

Ripoti iliyobainisha makosa hayo ya Muhimbili tayari CAG Charles Kichere aliiwasilisha bungeni jijini Dodoma Aprili 6, 2023 ikigusa sekta mbalimbali ikiwemo utendaji wa mashirika ya umma.

Kupitia ripoti hiyo, dosari ya MNH inaifanya kukosa ulinzi wa kisheria endapo kutatokea mgogoro na watu hao.

“Mapungufu haya yanatokana na hospitali kushindwa kupitia na kuhuisha mikataba na kutokuwepo kwa usimamizi thabiti wa mikataba kuhakikisha huduma za mikopo zinatolewa kwa wateja wenye mikataba.

Ninapendekeza Hospitali ya Taifa Muhimbili ipitie mikataba yote iliyoisha muda ili kuihuisha, na kuhakikisha huduma za mikopo zinatolewa kwa wateja wenye mikataba,” amependekeza CAG katika ripoti hiyo ya ukaguzi wa mashirika ya umma.

Kuhusu hatua za kunusuru fedha hizo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano MNH, Neema Mwangomo alipotafutwa kwa njia ya simu na ujumbe mfupi akifahamishwa juu ya kilichobainishwa kwenye ripoti hiyo ya CAG kwa njia ya ujumbe mfupi aliandika yupo kanisani.