Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ripoti ya CAG yabaini Sh77.5 bilioni zatumika isivyostahili

Muktasari:

  • Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imeyataja mashirika 21 yaliyotumia Sh77.5 bilioni isivyostahili.

Dar es Salaam. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 mashirika 21 ya umma yametumia Sh77.75 bilioni, ikiwa ni matumizi yasiyostahili, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imebainisha.

Ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma jana Alhamisi 6, 2023 imehusisha ukaguzi wa mwaka wa fedha 2021/22 katika maeneo mbalimbali yakiwemo mashirika ya umma.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, matumizi hayo yalitokana na malipo ya posho kwa watumishi wasiostahili, malipo yasiyokuwa na uthibitisho na vielelezo vya matumizi husika.

Katika ripoti yake hiyo, Kichere ameitaja Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuwa shirika kinara kwa matumizi hayo, likiwa likitumia Sh65.33 bilioni.

Mashirika mengine ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS), lililotumia Sh 8.598 bilioni, Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Sh2.42 bilioni na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania Sh489 milioni.

Mengine ni Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Sh237.7 milioni, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Sh150.3 milioni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) Sh111.25 milioni na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Sekta Binafsi Sh59.33 milioni.

Pia, umo Mfuko wa Maendeleo ya Zao la Pamba Sh50 milioni, Shrika la Umeme Tanzania (Tanesco) Sh48.59 milioni, Chuo cha Uhasibu Arusha Sh41.1 milioni na Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam Sh32 milioni.

“Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Ruwasa) Mwanza Sh56.78 milioni, Bodi ya Nyama Tanzania Sh29.4 milioni, Ruwasa Tabora Sh23.12 milioni, Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) Sh15.93 milioni na Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo (Sido) Sh11.79 milioni,” imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Sh11.52 milioni, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam Sh6.07 milioni, Chuo cha Diplomasia Sh5.5 milioni na Kampuni ya Mbolea Tanzania Sh4.8 milioni.

Kutokana na matumizi hayo, CAG Kichere amependekeza mashirika hayo kurudisha fedha zote katika maeneo husika.