Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto mahakamani kwa kumnyonga mwenzake

New Content Item (1)
Mtoto mahakamani kwa kumnyonga mwenzake

Muktasari:

Mtoto wa miaka 15 aliyekuwa akifanya kazi za ndani amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akikabiliwa na shtaka la mauaji ya mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Arusha. Mtoto wa miaka 15 aliyekuwa akifanya kazi za ndani amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akikabiliwa na shtaka la mauaji ya mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Amefikishwa mahakamani leo Ijumaa Julai 9, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Salome Mshasha huku upande wa jamhuri ukiwakilishwa na wakili, Blandina Msawa .

Mtoto huyo amesomewa shtaka moja la mauaji ya kukusudia kinyume na sheria katika shauri ambalo halikuwa la wazi kutokana na umri wa mtuhumiwa.

Msawa ameieleza mahakama kuwa Juni 19, 2021 eneo la Olkerian kata ya Olasiti kinyume na sheria alimuua mtoto wa bosi wake kwa kumnyonga shingo na hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi  Julai 19, 2021  itakapotajwa tena kutokana na upelelezi wake kutokukamilika huku mtoto huyo akipelekwa gerezani.