Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msongo wa kilovolti 132 kumaliza tatizo la umeme Tabora

Mafundi wakitengeneza miundombinu ya  mradi wa umeme wa Tabora - Katavi uliokamilika na utanufaisha wakazi wa Wilaya ya Tabora, Urambo na Kaliua.

Muktasari:

  • Wakazi wa Tabora, Urambo na Kaliua watanufaika na upatikanaji wa umeme wa uhakika baada ya kuwashwa kwa laini ya msongo wa kilovolti 132 yenye urefu wa kilomita 115,  mradi uliogharimu Sh40 bilioni.

Dar es Salaam. Wananchi wa mkoa wa Tabora wataepukana na changamoto ya umeme baada ya kuwashwa rasmi laini ya msongo wa kilovolti 132 yenye urefu wa kilomita 115.

Mradi ulianza Aprili 2024 na ulitegemewa  kumalizika Juni 2025.

Mradi huo utasaidia kuchochea maendeleo katika  Wilaya ya Urambo, Kaliua na Mkoa wa Tabora kwa ujumla.

Akizungumza leo Machi 20, 2025 mkoani Tabora katika shughuli ya kuwasha laini hiyo, Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya  wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme ( ETDCO), Sadock Mugendi amesema wategemee kupata umeme wa uhakika.

"Licha ya uhakika wa kupatikana kwa umeme pia mradi huu umetekelezwa na wataalamu wazawa, jambo ambalo limeonyesha tunaweza kutekeleza miradi ya umeme kwa wakati bila tatizo lolote," amesema Mugendi.

Amesema wameshukuru kumaliza mradi huo kabla ya wakati ili wananchi waweze kupata umeme wa uhakika haraka iwezekanavyo.

Meneja wa Mradi wa Tabora - Katavi kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Sospeter Oralo amesema mradi huo umegharimu Sh40 bilioni.

Amesema gharama ya laini yya Kilovolti 132 kutoka Tabora hadi Urambo ni Sh24 bilioni huku ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Urambo zimetumika Sh16 bilioni.