Mradi wa umeme wa Backbone kukamikilia Septemba

Muktasari:
Mradi huo ulioanzia Mkoa wa Iringa hadi Shinyanga utakuwa na msongo wa kilovolti 400, umbali wa kilomita 670. Kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni fursa kwa viwanda kupata umeme mkubwa na wa uhakika.
Iringa. Awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Backbone utakaounganisha nchi za Zambia na Kenya unatarajiwa kukamilika Septemba, mwaka huu na kuiwezesha Tanzania kuwa na umeme wa uhakika.
Mradi huo ulioanzia Mkoa wa Iringa hadi Shinyanga utakuwa na msongo wa kilovolti 400, umbali wa kilomita 670. Kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni fursa kwa viwanda kupata umeme mkubwa na wa uhakika.
Meneja wa Mradi wa Backbone, Mhandisi Oscar Kanyama amesema mradi huo unafadhiliwa na mashirika mbalimbali ambayo ni Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Maendeleo la Japan (Jica).
Kanyama amesema mradi huo unatarajiwa kuanza kutumia umeme huo ifikapo Septemba.
Hata hivyo, amesema kipande cha Iringa – Dodoma kinachofadhiliwa na WB kwa thamani ya Dola za 134.5 milioni za Marekani kimekamilika na kitaanza kutumika mwishoni kwa mwezi huu.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz