Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto uliowaka kwa siku 7 Kilimanjaro wadhibitiwa

Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Angela Nyaki akitoa taarifa ya udhibiti wa moto katika hifadhi hiyo.

Muktasari:

  • Moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana, ulianza kuwaka septemba 3, mwaka huu, ambapo eneo lililoungua ni ukanda wa juu, kaskazini mashariki mwa hifadhi ambapo ni umbali wa zaidi ya mita 3,900 kutoka usawa wa bahari.

Rombo. Moto uliowaka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (Kinapa) katika eneo la Indonet-Rongai Wilaya ya Rombo, umedhibitiwa kwa asilimia 90, huku eneo lenye ukubwa wa Kilometa za mraba 17 sawa na asilimia 0.9 ya eneo lote la hifadhi, likiathiriwa na moto huo.

Moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana, ulianza kuwaka septemba 3, mwaka huu, ambapo eneo lililoungua ni ukanda wa juu, kaskazini mashariki mwa hifadhi ambapo ni umbali wa zaidi ya mita 3,900 kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Rongai Wilaya ya Rombo, Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Angela Nyaki amesema eneo ambalo limeungua lina mimea jamii ya Erika na majani ambayo ikishika moto inawaka kwa kasi.

“Moto huo ulianza Septemba 3, mwaka huu mchana, ambapo tulipata taarifa kutoka kwa mtumishi wa TFS Rongai na tulituma kikosi siku ile ile na sasa wako watu 83 ambao wanaendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo ambao tayari tumeudhibiti kwa asilimia 90,”amesema Nyaki.

Ameongeza kuwa “Eneo lililoungua ni kilometa za mraba 17 sawa na asilimia 0.9 ya eneo lote la hifadhi, na eneo lolote dogo linaloungua kwetu ni hasara kwa sababu ya utalii na uoto ambao wageni wengi wakija wanapenda kuuona,”

“Ukanda ulioungua ni ukanda wa kaskazini Mashariki mwa hifadhi,ni eneo ambalo tunapakana na Nchi ya Kenya, na ni ukanda wa juu ambao umeathirika zaidi, tunapambana moto usiende juu sana wala usishuke chini ili usilete madhara kwenye msitu”.

Kwa upande wake Afisa uhifadhi Mkuu Kinapa, Mapinduzi Boniphace amesema moto huo umewaka kwenye vijiji vitatu ambapo ni Rongai, Indoneti mpaka Kamwanga na kwamba wamepeleka vikosi kutumia njia tofauti ili kuhakikisha kila eneo ambalo moto upo unadhibitiwa.

Boniphace amesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi wanaoishi vijiji vya kuzunguka eneo hilo, kujitokeza kushiriki kuuzima moto huo, jambo ambalo limeleta mafanikio makubwa katika kuudhibiti.