Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge CCM adai Katiba mpya bungeni

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina

Muktasari:

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina ameibua sakata la mchakato wa Katiba mpya ndani Bungeni akihoji kuna hatua gani za maandalizi Serikali imefikia.


Dodoma. Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina ameibua sakata la mchakato wa Katiba mpya ndani Bunge akihoji kuna hatua gani za maandalizi Serikali imefikia.

Mpina ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 8, 2023 wakati akichangia taarifa za kamati ya sheria na sheria ndogo akisema Serikali inamkosea Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alishatangaza kukubali kutunga Katiba mpya au kufanya marekebisho kwa katiba iliyopo.

Hoja ya kudai Katiba mpya imepelekwa bungeni kwa mara ya kwanza na mbunge wa CCM kwani wakati wote imekuwa ikitajwa na wabunge kutoka vyama vingine nje ya chama hicho tawala.

Mbunge huyo aliyewahi kuwa waziri wa mifugo na uvuvi amesema Katiba iliyopo haina nguvu ya kusimamia rasilimali za fedha ndiyo maana kumekuwa na alichokiita tobo la mali za umma.

"Rais Dk Samia Suluhu Hassan alisharidhia kufanya marekebisho ya Katiba au kutungwa lakini miezi sita hadi saba hakuna maandalizi yoyote yanayofanyika, hapo mnamkwamisha Rais wetu," amesema Mpina.

Amesema matobo ya mikataba mikubwa ikiwemo kipande cha Ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora, Bwawa la Mwalimu Nyerere na hukumu ya Trab na Tract kwamba zimetokana na ubovu wa Katiba ya sasa.

Amewataka wabunge kukataa mpango huo na kuomba marekebisho ya Katiba yafanyike ili kuziba mianya iliyopo.

Mpina ameomba Bunge liongeze Azimio la kuitaka Serikali ipeleke bungeni taarifa za kesi zote ambazo imeshindwa na kiasi inachodaiwa lakini sababu zielezwe kama walivyoelezwa kuwa Serikali imeokoa Sh13. 33 trilioni katika kesi za madai.