Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maofisa watendaji watatu Halmashauri ya Kilindi wafikishwa mahakamani

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Maafisa watendaji watatu katika halmashauri ya Wilaya ya Kilindi leo wamefikishwa na Takukuru katika mahakama ya Wilaya ya Kilindi wakikabiliwa na mashtaka ya kupoteza makusanyo ya halmashauri.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, leo Alhamisi Juni 22, 2023 imewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Kilindi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi waliopewa kazi ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine za POS.

Waliofikishwa mahakamani hapo ni wakusanyaji mapato ambao hawakuweza kuwasilisha makusanyo ya mapato kwa Afisa Mapato Wilaya ya Kilindi kinyume na Kanuni za Fedha za Serikali za Mitaa za mwaka 2009.

Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka na Mwendesha mashtaka wa serikali, Frank Pastory Maugo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kilindi, Musa Ngalu.

 Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka matatu; ambayo  ni ufujaji na ubadhirifu wa mali ya umma kinyume na vifungu vya 28(1) vya sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 sura ya 329 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Shtaka jingine ni wizi kwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 270 na 265 ya sheria ya makosa ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022  tatu ni kuisababishia hasara Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi kwa kutowasilisha makusanyo ya mapato kwa mhasibu wa halmashauri kinyume na aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) ya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya 2022.

Mshtakiwa wa kwanza ni Joyce Ikungu ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji cha Songe  aliyefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi EC. namba  8/2023 kwa kuisababishia hasara ya kiasi cha Sh3,590,00 Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi wakati akitimiza jukumu la ukusanyaji mapato ya Halmashauri hiyo.

Mshtakiwa wa pili ni Calvin Ombeni Lema Mtendaji Kata ya Kimbe ambaye amefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi EC. namba  6/2013 kwa kuisababishia hasara halmashauri kiasi cha Sh4,528,100.

Mshtakiwa wa tatu ni Athumani Mohamed Mhina Mtendaji wa kijiji cha Masagalu ambaye amefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi EC. Na 7/2023 kwa kusababisha hasara ya Sh1,415,200, kwa halmashauri ya Wilaya ya Kilindi wakati wa utekelezaji jukumu la ukusanyaji mapato.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote mpaka kesi itakaposomwa tena Juni 27, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Kilindi, washitakiwa wote wameachiwa huru kwa dhamana.