Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda awavaa watendaji wa Serikali

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda akizungumza katika hafla ya ukaribisho wake katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha na Sunday George

Muktasari:

  • Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amewataka watendaji wote wa Serikali kuwajibika ipasavyo katika nafasi na majukumu yao huku akisema hatakuwa tayari kubeba msalaba wa mtu

Dar es Salaam. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amewataka watendaji wote wa Serikali kuwajibika ipasavyo katika nafasi na majukumu yao huku akisema hatakuwa tayari kubeba msalaba wa mtu.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema angeshaangaa kama kiongozi huyo mpya kwenye chama, asingetoa kauli hiyo, akiamini kuwa ili chama hicho kiendelee kuaminiwa na Watanzania, ni lazima watekeleze ilani ya chama hicho kwa kujibu kero wanazopitia.

"Nimesikiliza hotuba yake aliyoyasema ni ukweli kwani ana nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya chama, na ili kiweze kuendelea kuaminiwa, ni lazima ahadi zilizotolewa kupitia ilani, zitekelezwe," amesema bosi huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye hafla ya mapokezi yake yaliyofanyika katika ofisi ndogo za chama hicho, Makonda ametaka Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini, kufanya kazi na kwamba watakaoshindwa, yeye hatakuwa tayari kuwa msemaji wa chama ambacho watendaji wake hawawajibiki.

"Kazi ya chama ni kuwa sikio na kuwasemea wananchi, naomba nitumie fursa hii kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutuma salama kwa Mawaziri wote, Wakuu wa Mikoa, wakiwakilishwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam na watendaji wote, pale itakapobainika hamjafanya kazi yenu kikamilifu chama hakitasita kuchukua hatua," amesema.

Amesema bahati nzuri anafahamika na watendaji wote hatakuwa tayari kuwa msemaji wa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi asimame hadharani kusema uongo.

"Kila kiongozi wa Serikali atabeba msalaba wake mwenyewe, sijahifadhiwa miaka mitatu kuja kusema uongo, sijateuliwa na CCM kuja kusema uongo na kauli iko wazi, uongo, fitina si sehemu ya chama nitakuwa mkweli daima," amesema.

Makonda ambaye pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kiongozi yeyote atakaye bainika hatendi sawa na kwamba chama kikajiridhisha, hawatachelewa kuchukua hatua, huku akiwaka kibwagizo cha sheria za katika Msikiti isivyoruhusu mtu kuingia na viatu na kwamba akibainika, haitamngojea Imam kuchukua hatua dhidi ya mtu huyo.

"Tutachukua hatua bila kusubiri, kwa kiongozi yeyote atakaye rudisha nyuma jitihada za chama kuendelea kuaminiwa na wananchi," amesema.