Mafuru: Serikali ndiyo inayoua taasisi zake

Muktasari:
- “Taasisi na mashirika ya umma yanakufa kutokana na kuidai Serikali madeni makubwa ambayo hayalipwi,” alisema Mafuru.
Dodoma. Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru amesema muuaji wa taasisi za umma ni Serikali yenyewe kwa kutolipa madeni yanayotokana na huduma wanazopatiwa.
Mafuru amesema hayo wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokutana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (Duwasa) katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini hapa.
“Taasisi na mashirika ya umma yanakufa kutokana na kuidai Serikali madeni makubwa ambayo hayalipwi,” alisema Mafuru.