Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jalada la aliyekuwa mkurugenzi NIC, wenzake lafanyiwa marekebisho

Muktasari:

  • Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili wafanyakazi wa Shirika la la Bima la Taifa (NIC) umedai kuwa wamebaini kuna nyaraka hazijawekwa hivyo wameomba jalada hilo lirudishwe ili waweze kufanya marekebisho na kuziwasilisha upya taarifa hizo Mahakama Kuu.

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Samweli Kamanga na wenzake sita umedai kuwa wanafanya marekebisho ya taarifa za kesi hiyo waliyoiwasilisha Mahakama Kuu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 365 yakiwemo ya kutakatisha fedha kiasi cha Sh1.8 bilioni mali ya NIC.

Wakili wa Serikali, Wini Samson alidai hayo leo Septemba 25, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Evodia Kyaruzi alidai hayo wakati shtaka hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa kuwa walibaini kuna nyaraka hazijawekwa tuliomba jalada lirudishwe ili waweze kulifanyia marekebisho.

"Ni kweli kwamba hapo awali tulikuwa tumewasilisha taarifa  za kesi hii Mahakama Kuu, lakini jalada lilivyoenda Mahakama Kuu tulibaini kuwa kuna nyaraka hazijawekwa tukaomba jalada lirudishwe hivyo tunaziandaa nyaraka  ili tuweze kufanya marekebisho na kuziwasilisha upya taarifa za jalada hilo Mahakama Kuu," alidai Samson.

Hakimu Kyaruzi aliaharisha kesi hiyo hadi Octoba 10, 2023 kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Kamanga wengine ni Tabu Kingu, Victor Mleleu, Peter Nzunda, Kenan Mpalanguro, Lusubilo Sambo na Mafworo Ngereji.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi 2013 na Desemba 31, 2018 katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, mkoani Rukwa, Kilimanjaro,  Arusha, Mbeya, Morogoro na Kigoma washtakiwa hao walioongoza genge la uharifu na kujipatia Sh1 bilioni mali ya NIC.

Inadaiwa katika kipindi hicho washtakiwa kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu  ili kujipatia Sh1.8 bilioni kwa njia ya ulaghai kutoka Shirika la Bima la Taifa.

Mashtaka mengine yanayowakabili washitakiwa hao ni ya kugushi hundi mbalimbali wakionesha ni halali zimetolewa na shirika hilo wakati wakijua siyo kweli.

Pia ilidaiwa kwamba, washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kuchepusha fedha, kuwasilisha nyaraka za kughushi kwa lengo la kujipatia fedha, utakatishaji fedha ambapo miongoni mwao walidaiwa kutumia fedha hizo kununua viwanja, ardhi zisizopimwa na magari.