Mwelekeo mpya kesi ya vigogo NIC

Muktasari:
- Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema wanasubiri jalada kutoka Mahakama Kuu ili shauri liweze kwenda mbele katika kesi inayowakabili watumishi saba wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Sam Kamanga.
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema wanasubiri jalada kutoka Mahakama Kuu ili shauri liweze kwenda mbele katika kesi inayowakabili watumishi saba wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Sam Kamanga.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 390, likiwemo la kuchepusha fedha na kuisabishia shirika hilo hasara ya zaidi ya Sh 1.8 bilioni.
Kyaruzi alisema hayo leo Septemba 11, 2023 kuwa mahakama hiyo inasubili jalada kutoka Mahakama Kuu kwa kuwa upande wa mashtaka walishawasilisha taarifa katika Mahakama hiyo.
"Tunasubili jalada kutoka Mahakama Kuu ili shauri hili liweze kwenda mbele kwa kuwa upande wa mashtaka walishawasilisha taarifa,"alisema Kyaruzi.
Awali Wakili wa Serikali,Winiwa Samson alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi alidai kuwa upelelezi umekamilika wamewasilisha taarifa Mahakama Kuu hivyo ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe ya kutajwa.
Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 25, 2023 Kwa ajili ya kutajwa.
Inadaiwa kati ya Januari Mosi 2013 na Desemba 31, 2018 katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, mkoani Rukwa, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Morogoro na Kigoma washtakiwa kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia Sh 1.8 bilioni kwa njia ya ulaghai kutoka Shirika hilo.
Katika shtaka la kughushi, linalomkabili Kingu na Nzunda, Oronu inadaiwa Mwaka 2013 katika Wilaya ya Ilala, washtakiwa hao wakiwa wahasibu, walighushi hundi yenye thamani ya Sh50 milioni wakionyesha kuwa kuwa ni halali na imetolewa na NIC.
Inadaiwa katika mashtaka ya utakatishaji washtakiwa Maleleu, Nzunda, Mparanguro, Sambo na Oronu walijihusisha kununua mashamba na magari maeneo tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, mkoani Rukwa, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Morogoro na Kigoma huku wakijua fedha hizo ni mazalia yq makosa ya jinai.