Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hukumu wanaodaiwa kutapeli kwa jina la Waziri Mkuu Novemba 30

Muktasari:

  • Mahakama itatoa hukumu hiyo kwa washtakiwa wanaodaiwa kumtapeli raia wa China Dola 10,000 kwa kujitambulisha kuwa ni katibu muhtasi wa Waziri Mkuu.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imepanga Novemba 30, 2023 kutoa hukumu katika kesi ya kujipatia Sh22 milioni inayomkabili Bahati Maliwa (50) na Godfrey Mtonyi (30).

 Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka sita, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 14 ya mwaka 2020, iliyopo mahakamani hapo.

Wanadaiwa kujipatia fedha hizo baada ya Malila kujitambulisha kwa mfanyabiashara na raia wa China, Biao Lin Tang, kuwa ni katibu muhutasi wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akijua ni uongo.

Katika mashtaka yao; yapo kughushi nyaraka, kuwasilisha nyaraka za uongo wakionyesha zimetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na kujipatia dola 10,000 kwa udanganyifu ambazo ni sawa na zaidi ya Sh22 milioni kwa kipindi hicho ikiwa ni mali  Biao Lin Tang.

Uamuzi huo umetolewa leo, Novemba 27, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kufunga ushahidi wao.

Okotoba 19, 2023 Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu washtakiwa hao baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 10, huku upande wa utetezi ukiwasilisha mashahidi wanne wakiwemo washtakiwa wenyewe.

Hakimu Kabate baada ya kueleza hayo, ameahirisha kesi hadi Novemba 30, 2023 itakapotolewa hukumu.

Miongoni mwa mashahidi katika kesi hiyo ni Lin Tang, mfanyabiashara na raia wa China.

Lin Tang, katika ushahidi wake ameieleza Mahakama jinsi alivyotapeliwa fedha hizo, baada ya Malila kujitambulisha ni katibu muhutasi wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akijua ni uongo.

Lin Tang ambaye ni Rais wa Taasisi ya Canton HongKong and Macau Fellow Townsmen Association in Tanzania, amedai taasisi yake ilipanga kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa msaada katika Jimbo la Ruangwa ambalo Majaliwa ndiye mbunge, walipanga kutoa dola 20,000 kwa ajili ya kuwanunulia watoto wenye uhitaji vifaa mbalimbali vya shule ikiwemo madaftari, vitabu, kalamu na sare za shule.

Amedai ili kufanikisha jambo hilo, alimshirkisha rafiki yake, John Kilasile kisha akamkutanisha na Malila ambaye alijitambulisha kama katibu muhutasi wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


 “Nikiwa Rais na mwenyekiti wa Taasisi ya Canton HongKong and Maccaw Fellow Townsmen Association in Tanzania, niliita wanachana wote na msaidizi wangu  na kufanya kikao cha kusaidia watoto hao katika Jimbo la Ruangwa,” amesema Lin Tang.

Amedai baada ya kikao hicho, walikutana kwa mara ya pili na kufanya kikao kidogo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kilichohusisha watu watano akiwepo yeye, John Kilasile, Bahati Malila, msaidizi wa Jin Tang ambaye ni  Guanhui Su Biaolin Tang na mwanamke mmoja ambaye hakumfahamu ila alitambulishwa kama rafiki wa Kilasile.

Katika kikao hicho, walimueleza Malila kuwa wana Dola 20,000 ambazo zinatakiwa kutolewa katika Jimbo la Ruangwa pamoja na vifaa vya shule ikiwemo sare za shule, madaktari, kalamu kwa ajili ya kusaidia watoto yatima wanaosoma katika Jimbo hilo.

Lin Tang amedai Malila alimueleza shahidi huyo kuwa hitaji la kwanza ili kazi hiyo ifanikiwe alimtaka atoe Dola 10,000 ili apate vyeti vitatu ikiwemo cheti cha shukrani kinachoonyesha wanachokwenda kufanya ni chema katika Jimbo la Ruangwa.

“Bahati aliniambia, cheti cha kwanza kitakuwa na jina langu, cheti cha pili kitakuwa na jina la msaidizi wangu na cha tatu kitakuwa na jina la taasisi yetu,” amedai shahidi huyo.

Hata hivyo, Lin Tang alitoa dola 10,000 na kumpa Malila ili atengeneze vyeti hivyo.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa Januari 13, 2020 katika eneo la Msasani, Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wakiwa na nia ovu walighushi vyeti vitatu wakionyesha vya kuchangia michango kwa ajili ya kutoa misaada elimu kwa watoto wenye uhitaji, vikionyesha vimetolewa Januari 13, 2020 na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa, wakati wakijua ni uongo.

Katika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka zilizoghushiwa, inadaiwa Januari 14,2020 washtakiwa wakiwa wanafahamu na kwa nia ovu waliwasilisha nyaraka za uongo kwa Biao Lin Tang ambazo ni vyeti vya utoaji wa michango kwa ajili ya misaada vikionyesha kuwa vimetolewa na Januari 13, 2020 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wakijua ni oungo.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, washtakiwa wanadaiwa, Januari 14, 2020 katika eneo la Msasani, Kinondoni, walijipatia Dola 10,000 (Sh22,950,000) kutoka kwa Biao Lin Tang kwa kudai zinakwenda Jimbo la Ruangwa ambalo linasimamiwa na Majaliwa kwa ajili ya ununuzi wa vifa vya shule, wakijua kwamba si kweli.