Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hospitali binafsi zatangaza kusitisha huduma wanachama NHIF

Muktasari:

  • Wakati sakata hilo likipamba moto, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameahidi kulitolea suala hilo ufafanuzi kesho Ijumaa, Machi Mosi.

Dar es Salaam. Kauli ya pamoja ya Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya nchini Tanzanja (Aphfta)  kusitisha huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imeanza utekelezaji baada ya baadhi ya hospitali kubwa za binafsi kuanza kutoa taarifa rasmi.

Vituo vilivyotoa taarifa kupitia mtandao ni pamoja na Hospitali ya Kairuki, Hospitali ya Regency na Hospitali ya TMJ za jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo inafuatia tamko lililotolewa leo Alhamisi, Februari 29, 2024 na Mwenyekiti wa Aphfta, Dk Egina Makwabe alipoeleza msimamo wao kuhusu kutokubaliana na mabadiliko yaliyofanywa na kuanza kwa kitita kipya cha gharama za matibabu kwa wanachama wa mfuko huo.

Wakati sakata hilo likipamba moto, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameahidi kulitolea suala hilo ufafanuzi kesho Ijumaa, Machi Mosi.

Taarifa iliyosambazwa na msemaji wa Hospital ya Kairuki usiku huu, imeeleza;

"Uongozi wa Kairuki Hospital unapenda kuwafahamisha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwamba kuanzia Machi Mosi saa 6 usiku watutatoa huduma kwa wanachama hao mpaka utaratibu mpya wa kuwapokea utakapojulikana," imeeleza taarifa hiyo.

Aidha imeeleza uongozi wa Kairuki unawashauri wanachama hao kuwasiliana na NHIF ili kujua namna watakavyoendelea kupata huduma.

"Wateja wetu wanaweza kuendelea kupatiwa huduma kwa kutumia bima nyingine zinazopokelewa Kairuki Hospital au kulipa pesa taslimu," imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa nyingine iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ya Hospital ya Regency, pia imeeleza kusitisha huduma kwa wateja wake wanaotumia NHIF.

Taarifa nyingine inayosambaa mtandaoni ni ya Hospital ya TMJ inayosema;

"Uongozi wa kituo unapenda kuwafahamisha wanachama wa bima ya afya ya Taifa NHIF kwamba kuanzia Machi Mosi saa 6:01 usiku hatutapokea huduma kwao mpaka utaratibu maalum wa kuwapokea utakapojulikana," umeeleza ujumbe huo ukiwataka wanachama hao kuwasiliana NHIF.

Wakati hayo yakijiri, Jumatano ya Februari 28, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alitaja manufaa ya kitita hicho kipya kuwa ni

kwa wanachama wanaotumia dawa za pressure na sukari sasa wanaweza kupata dawa ngazi za chini

Pia, alitaja faida zingine kuwa wanachama wenye magonjwa sugu ya figo wanaopata huduma ya kuchuja damu gharama imeshushwa chini.

"Huduma za kibingwa na bingwa bobezi kama matibabu ya moyo, saratani, figo sasa zitapatikana kwenye ngazi za kanda pia na sio lazima mwanachama aende mpaka hospitali za ngazi ya taifa pia dawa 247 mpya zimeongezwa kwenye kitita," alisema Konga.