Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gwajima alikuja kwa dharau na kejeli - Mbunge CCM

Muktasari:

  • Mbunge wa Kilindi (CCM) nchini Tanzania, Omary Kigua amesema ujio wa Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu shauri lake la kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge ulikuwa wa dharau na kejeli.

Dodoma. Mbunge wa Kilindi (CCM) nchini Tanzania, Omary Kigua amesema ujio wa Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu shauri lake la kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge ulikuwa wa dharau na kejeli.


Kigua ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 31, 2021 wakati akichangia katika ripoti ya kamati hiyo kuhusu shauri la mbunge huyo.

Amesema wameshuhudia vituko katika kamati hiyo na kwamba vitendo vya mbunge huyo havifanani na nafasi aliyonayo katika Bunge.

“Shahidi (Gwajima) hakuitendea haki hakuwa na nidhamu, heshima na hata ujio wake katika kamati ulikuwa wa dharau na kejeli uliopitiliza,”amesema Kigua.
Mwisho