Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatima usikilizwaji kesi ya Lissu kujulikana Mei 6

Muktasari:

  • Hakimu amepanga tarehe hiyo, baada ya Serikali kumaliza kujibu hoja zilizowasilishwa na mawakili wa Lissu.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Mei 6, 2025 kutoa uamuzi iwapo kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa YouTube inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, iwapo itaendeshwa kwa njia ya mtandao au mshtakiwa huyo ataletwa mahakamani hapo.

Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatatu Aprili 28, 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini, wakati kesi hiyo iliposikilizwa kwa njia ya mtandao.

Hakimu Mhini amepanga tarehe hiyo, baada ya Serikali kumaliza kujibu hoja zilizowasilishwa na mawakili wa Lissu.

"Baada ya upande wa mashitaka  kumaliza kujibu hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi, inabidi na mimi nipate muda wa kupitia hoja zote na Mei 6, 2025 nitatoa uamuzi kwa njia ya mtandao," amesema Hakimu Mhini.

Awali,  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema aliieleza mahakama hiyo kwa njia ya mtandao  kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya upande wa mashitaka kujibu hoja zilizowasilisha na mawakili wa Lissu na wapo tayari.

Baada ya kueleza hayo, Job alianza kujibu hoja hizo kwa njia ya mtandao huku mawakili wa Lissu wakiongozwa na Dk Rugemeleza Nshala wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Mahakama hiyo ambao unatumika kwa ajili ya kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao.

Kwa mara ya kwanza, Lissu alipandishwa mahakamani Aprili 10, 2025 na kusomewa kesi ya jinai yenye mashitaka matatu ya kutoa taarifa za uongo.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mshtakiwa alikana kutenda na Serikali iliieleza Mahakama upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na ukaomba Mahakama ipange tarehe kwa ajili ya usikilizwaji wa hoja za awali (PH).

Hivyo Mahakama hiyo ilipanga kuendelea na hatua hiyo Aprili 24, 2025.

Hata hivyo siku hiyo kesi hiyo haikuendelea katika hatua hiyo baada ya Lissu kugomea utaratibu uliowekwa na Mahakama, kusikiliza kesi hiyo kwa njia ya mtandao (video conference), huku akiwa mahabusu katika Gereza la Ukonga.

Lissu aligoma kwenda katika chumba chenye mawasiliano hayo katika gereza hilo na badala yake alitaka afikishwe mahakamani kesi yake isikilizwe katika Mahakama ya wazi na kutoa fursa kwa umma kuifuatilia.

Jopo la mawakili wanaomwakilisha Lissu zaidi ya 31, likiongozwa na Wakili Mpale Mpoki na wengine wakiwemo Dk Rugemeleza Nshala, Peter Kibatala na kaka  yake Lissu, Alute Mughwai, Jeremiah Mtobesya liliunga mkono msimamo huo wa mteja wao.

Mawakili hao pamoja na mambo mengine walidai utaratibu huo  ni kinyume na matakwa ya  sheria, kwani katika hatua hiyo ya usikilizwaji wa awali mshtakiwa anapaswa kufikishwa mahakamani.