Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Falsafa ya 4R, mwelekeo wa maendeleo

Rais Samia Suluhu Hassan amesema alipoingia madarakani aliona haja ya kuhakikisha wanaendelea kujenga Taifa la maelewano na maridhiano ili kwenda pamoja katika mwelekeo wa maendeleo.

“Dhima hii ilinisukuma kubuni na kutekeleza falsafa ya 4R, tukiongozwa na falsafa hiyo ilituelekeza kwenye mageuzi, maridhiano, ustahimilivu na kujenga upya,” amesema hayo leo Juni 27, 2025 bungeni jijini Dodoma alipolihutubia kuhitimisha shughuli za Bunge la 12.

Amesema: “Tuliweza kuwaleta wadau wa kisiasa na wengine pamoja na kufanya uamuzi na maboresho mbalimbali yaliyojumuisha na kushirikisha wadau wote.”

Samia amesema Serikali iliunda Tume ya Maridhiano iliyofanya kazi nzuri ya kuja na mapendekezo ya muda mrefu na mfupi.
“Katika kutekeleza mapendekezo ya tume, Serikali iliondoa zuio la mikutano kwa vyama vya siasa na wote tumeshuhudia vyama vikiendelea kufanya shughuli zake kwa uhuru, ikiwemo mikutano ya hadhara,” amesema.

Vilevile, Baraza la Vyama vya Siasa limefanya mikutano sita na kutoa mawazo na ushauri uliowasilishwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Kuhusu Muungano, amesema ufumbuzi wa hoja 15 umeongeza imani ya Watanzania kwa Serikali.

“Pamoja na hayo niwaase Watanzania wenzangu tuendelee kushikamana na kuwa makini na vitisho vyovyote dhidi ya Muungano wetu. Niwasihi pia kuendeleza utulivu na amani vitu ambavyo ni sifa njema kwa nchi yetu,” amesema.