Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Faida ya kuoga maji ya baridi

Muktasari:

Katika kipindi hiki cha msimu wa baridi nchini, baadhi ya watu wamepunguza matumizi ya maji kwenye miili yao kwa maana suala zima la kuoga limekuwa mtihani.

Katika kipindi hiki cha msimu wa baridi nchini, baadhi ya watu wamepunguza matumizi ya maji kwenye miili yao kwa maana suala zima la kuoga limekuwa mtihani.

Baadhi ya maeneo watu wanaona bora wasioge kutokana na baridi, lakini kiafya inaelezwa maji ya baridi yana faida hasa kwa watu wanaozingatia masuala ya urembo na utanashati.

Je uko tayari kuongeza maarifa au hata kubadili mtazamo wako kuhusiana na maji ya baridi?

Kwanza maji ya baridi hukufanya uchangamke, hili ni tofauti na maji ya moto.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Thrombosis Research Institute, watu wanaooga maji ya baridi wanaongeza uzalishaji wa seli nyeupe za damu.

Utafiti huu unaeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha metaboli mwili unapojaribu kujipasha moto, ndipo seli hizi nyeupe ambazo hupambana na maradhi zinapozalishwa.

Kumbuka hata wakati wa kuoga maji baridi kasi ya upumuaji hubadilika na kukufanya kuongeza kiasi cha oksijeni mwilini.

Pia, hulainisha ngozi na nywele tofauti na ilivyo kwa maji ya moto ambayo huchubua ngozi, hasa kwa kuondoa mafuta laini yanayolinda ngozi na nywele na kuzifanya ziwe kavu.

Lakini unapokoga maji ya baridi, ngozi na nywele zako hazitapaushwa bali vitasafiwa na kuachwa katika hali nzuri ya kupendeza.