Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elimu afya ya uzazi kuwafikia vijana 13,800 Dodoma

Mkurugenzi wa taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumzia utekelezaji wa mradi wa Tanzafya kwa ajili ya kutoa elimu ya afya ya uzazi mkoani Dodoma, wakati uzinduzi leo jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Kufuatia ongezeko la wasichana wanaopata mimba za utotoni na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi, Ubalozi wa Ufaransa kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali wamenaizisha mradi wa Tanzafya utakaofikisha elimu hiyo kwa vijana.

Dar es Salaam. Vijana wapatao 13,800 mkoani Dodoma wanatarajiwa kupata mafunzo na ushauri kuhusu afya ya uzazi na haki zao kupitia mradi unaoitwa Tanzafya.

Akizungumza leo Juni 21 katika uzinduzi wa mradi huo, Balozi wa Ufaransa Tanzania, Nabil Hajlaoui alisema utatekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (Umati), Doris Mollel Foundation na Medicin du Monde.

“Sisi Ubalozi wa Ufaransa tunashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya ili kufikia malengo ya mradi huu,” alisema.

Akizungumzia malengo ya mradi huo, Mkurugenzi msaidizi wa afya za watoto na vijana wa Wizara ya Afya, Dk Felix Bundala amesema mradi huo umelenga kuwasaidia vijana kukabiliana na changamoto za afya za uzazi.

“Utawasaidia vijana kujikinga na huduma dhidi ya Virusi vya Ukimwi, kujikinga na mimba za utotoni katika umri mdogo na masuala ya ukatili wa kijinsia, masuala lishe na magonjwa ya kuambukiza, afya ya kili, vijana wa kiume na kike kuendelea na masomo na masuala ya kuwezeshwa kiuchumi na kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Umati, Suzanna Mkanzabi, alisema Mkoa wa Dodoma umechaguliwa kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha mimba za utotoni.

“Asilimia 23 ya wasichana mkoani Dodoma wanapata mimba za utotoni, kwa hiyo sisi tuliona mkoa huo unakua kwa kasi na kuna vyuo vingi, tukaona tuwekeze huko ili tuwape taarifa kwa sababu hawana taarifa sahihi, ili waweze kujikinga,” alisema.

Naye MNkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel amesema taasisi yake inakusudia kuandaa filamu za mafunzo.

“Sisi jukumu letu kwenye huu mradi ni kuandaa filamu fupi zenye malengo ya kuangazia changamoto ambazo vijana wanapitia hususani masuala ya afya ya uzazi.

“Tutaangalia maeneo maeneo makuu mawili ambayo ni pamoja na ukatili wa kijinsia na uzazi wa mpango. Tutatengeneza maudhui yanayoakisi maisha yetu Watanzania,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Medicin du Monde (Tanzania), Ivan Duran ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushiriki katika miradi ya afya.