Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Shein atamani wazee kutunzwa

Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein

Muktasari:

Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (2010-2020), Dk Ali Mohamed Shein amesema suala la kuwatunza wazee ni jukumu la pande zote hivyo halikwepeki.

Dodoma. Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema suala la kuwatunza wazee ni jukumu la pande zote hivyo halikwepeki.

 Dk Shein ametoa kauli hiyo leo Septemba 29, 2022 jijini Dodoma, wakati akifungua mjadala kuhusu wazee unaondeshwa na Shirika la HelpAge na Taasisi ya Mwalimu Nyerere. Oktoba 1 ya kila mwaka huwa ni siku ya wazee duniani.

Rais huyo mstaafu amesema ni wakati wa Serikali na wanajamii kuungana pamoja kuwasaidia wazee kwa kuwa bila wao nchi isingekuwa mahali pazuri kama ilivyo kwa sasa.

"Ni lazima tuwatambue wazee kuwa wana umuhimu mkubwa, lazima tukubali kwamba jukumu la kuwalea ni letu sote bila kukwepa," amesema Dk Shein.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Serikali ya awamu ya kwanza kwa Tanzania ilishawatambua na kutolea mfano wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Abed Aman Karume ambaye aliwajengea nyumba za kuishi zenye hadhi nzuri wakati Taifa lilikuwa bado changa.

Katika utawala wake Zanzibar, Dk Shein alianzisha mpango wa kuwalipa pensheni wazee kwa kila mwezi utaratibu ulioendelezwa na Dk Hussein Mwinyi.