Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Nassoro: Uzazi wa mpango ni ajenda ya Serikali

Mkurugenzi msaidizi wa afya ya uzazi na mama, Dk Mzee Nassoro.

Muktasari:

  • Mkurugenzi msaidizi wa afya ya uzazi na mama, Dk Mzee Nassoro ameshiriki mjadala wa Mwananchi Space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd (MCL) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST) wenye mada ya ‘uzazi wa mpango ni hatua katika kufikia lengo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi? Na kueleza mikakati ya Serikali kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi wa mpango.

Dar es Salaam. Mkurugenzi msaidizi wa afya ya uzazi na mama, Dk Mzee Nassoro  amesema uzazi wa mpango ni ajenda ya Serikali katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

 Kauli hiyo ameitoa wakati akijibu maswali yaliyouzwa na wadau na wafuatiliaji mjadala huo umefanyika leo Jumatatu, Septemba 25, 2023 ambapo walikuwa wanataka kujua hatua za Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo nchini.

“Kundi la vijana linalojihusisha katika ngono, wengi wao wanapata mimba zisizotarajiwa huku wengine wakiishia kuzitoa na hatimaye kufariki dunia.

Tunapoboresha huduma zetu kwa kuondoa unyanyapaa kwa vijana katika huduma za uzazi wa mpango, tunategemea vifo vinavyotokana na uzazi au mimba zisizopangwa zitapungua,” amesema

Katika majibu yake, Dk Nassoro amesema hata suala la unyanyapaa Serikali si sera yake na kwamba watoa huduma wanapaswa kutoa taarifa huku akieleza wanajua kuna mimba za utotoni na kuna mikakati mingi ya kuzuia mimba za utotoni.

“…kutengeneza miundombinu ikiwemo kutoa elimu kwa vijana na kuto wanyanyapaa wanapokuja kutafuta huduma,” amesema

Katika maswali hayo, moja liliulizwa na Mwananchi, Fredy Kavishe akiomba kujua kuhusu unyanyapa unaofanywa na baadhi ya watoa huduma wa afya kwa mama ambaye mimba yake imeharibika, kwa  kutaka kujua mikakati ya kuboresha suala hilo.

Mkurugenzi huyo amebainisha madhara ya matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa kuwa ni njia zinazotumia homoni  zinachangamoto lakini inapotoka, mwili wa mama hurudi kwenye hali yake ya kawaida mathalani wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango.

“Atapata maudhi kidogo kama matiti kujaa, kusikia kichefuchefu na kuna homoni nyingine ataona mzunguko wake unaharibika lakini kuna vijiti na sindano ambapo huenda akaona ukeni kunakuwa kukavu na wakati mwingine tendo la ndoa kupotea,” amesema

Dk Nassoro amesema wanaopata madhara ni wachache mno ikilinganishwa na wanaopata faida na madhara hayo ukianza kutumia dawa huwa yanaacha moja kwa moja.

Amesema tatizo lingine wanaloliona akina mama wengi wanapotumia uzazi wa mpango huwa wanajiachia wanafanya ngono bila kuzingatia mambo mengine mathalani maambukizi.

“Kwa ujumla hatusemi hizi njia hazina madhara moja kwa moja hapana kuna madhara madogomadogo ambazo zinajitokeza na kuna baadhi  wanaopata uzito kupita kiasi na wakifanya utaratibu mwingine uzito huwa unapungua,”amesema