Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makwetta, Jhapiego wabainisha madhara, mikakati kupunguza vifo vya uzazi

Mwandishi wa masuala ya afya wa gazeti la Mwananchi, Herieth Makwetta.

Muktasari:

  • Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST) wameendesha mjadala wa X-Space wenye mada ya ‘uzazi wa mpango ni hatua katika kufikia lengo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi?’

Dar es Salaam. Mwandishi wa masuala ya afya wa gazeti la Mwananchi, Herieth Makwetta amesema jitihada zinahitajika za kutengeneza miundombinu ya kumwezesha mama mjazito kujifungua kwa wakati ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Makwetta amebainisha  leo Jumatatu, Septemba 25,2023 katika mjadala wa Mwananchi Space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd (MCL), wenye mada ya ‘uzazi wa mpango ni hatua katika kufikia lengo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi?.

Katika maelezo yake amesema mbinu hiyo itafikiwa endapo mama ataangaliwa namna gani atazaa kwa wakati, kwa maana ya kuachanisha kati ya mtoto mmoja hadi mwingine ili afya yake ikae vema kupokea mimba nyingine.

“Takwimu zinaonyesha mwaka 2012 vifo vilivyotokana na mama vilikuwa 432 kwa kila vizazi hai 100,000.Lakini mwaka 2015/16 vilipanda hadi kufikia 551 kwa kila vizazi hai 100,000. Hata hivyo lengo la Serikali ni kupunguza hivi vifo kutoka 551 hadi 292 kufikia mwaka 2025,” amesema

Katika mjadala huo, Mwananchi imeshirikiana na Wizara ya Afya pamoja Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Makwetta amesema ni wanawake wachache wanaoweza kufuatilia njia za asili kwa maana kalenda lakini wengi wao wanahitaji kupata njia za kisasa ili kuwa na uhakika kutoshika mimba nyingine wakati mtoto mwingine akiwa mdogo.

“Baadhi ya mikoa bado ipo nyuma katika matumizi ya uzazi wa mpango, nimetembelea kanda ya ziwa na kuona uwiano wa kuzaa watoto ni kati ya saba hadi nane, ukiangalia kuna visa vingi vya kina mama kupoteza maisha wakati wa kujifungua,”amesema

Kwa upande wake, Mshauri mwandamizi wa uzazi wa mpango wa shirika la Jhpiego, Dk Groly Shirima amesema wamekuwa wakishirikiana na Serikali kuhakikisha mitaala na miongozo inawaongoza watoa huduma kutoa njia sahihi za uzazi wa mpango.

“Jhapiego tupo katika mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ina vifo vingi vya mama na watoto na uhitaji wao wa njia za uzazi wa mpango ni kubwa, lakini tumejikita kuwajengea uwezo katika kuhakikisha watoa huduma wanazijua faida za uzazi wa mpango,” amesema

Amesema wamekuwa wakisisitiza huduma ya uzazi wa mpango baada ya kujifungua katika zahanati au vituo vya afya na watoa huduma wanawapa elimu ya matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango.

“Huwa wanafanya uamuzi baada ya kujifungua mama anapewa njia sahihi za uzazi wa mpango inayostahiki. Pia tumekuwa tukitoa msaada katika halmashauri tunazofanya nazo kazi, kwa kufika maeneo yasiyofika kupeleka huduma za uzazi wa mpango,” amesema.