Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Biteko awasilisha salamu za Rais miaka 61 ya Uhuru Uganda

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania bado inathamini mchango na maendeleo yaliyofikiwa na Uganda katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Kampala. Serikali ya Tanzania imeahidi kuendeleza ushirikiano, umoja na mshikamano na nchi ya Uganda kwa maslahi mapanga kwa mataifa yote mawili.

Mataifa hayo, licha ya kubadilisha vitu kwa wingi zaidi, ukichagizwa na ukaribu wao lakini historia ya uhusiano wao inajengwa zaidi na kumbukizi ya kihistoria ya 1979, Tanzania ilikuwa nchi pekee ya ukanda wa Afrika Mashariki iliyosimama na Uganda kuweka jitihada kupindua utawala wa kidikiteta wa Nduli Idd Amin Dada.

Akizungumza kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 61 ya nchi ya Uganda, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko aliyemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya Tanzania bado inathamini mchango na maendeleo yaliyofikiwa na taifa hilo katika utekelezaji wa miradi ya kiuchumi.

“Rais anaipongeza Uganda kwa siku hii muhimu ya miaka 61 ya Uhuru na wananchi wote na ameahidi kuendelea kushirikiana katika kujenga uchumi wa nchi hizi mbili na Afrika Mashariki kwa ujumla,” amesema Dk Biteko.

Katika hotuba yake aliyoitoa jana Oktoba 09, 2023 katika sherehe zilizofanyika viwanja vya Kitgum Kaskazini mwa nchi ya Uganda, Naibu Waziri Mkuu huyo amemshukuru Rais Yoweri Museveni kwa jitihada zake za kudumisha umoja na mshikamano kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kila awamu ya uongozi mathalani Tanzania, viongozi hao wamekuwa wakikubaliana kushirikiana, kibiashara na kuimarisha zaidi uhusiano wao hasa katika nyakati hizi mataifa hayo yanapokusudia kupiga hatua kiuchumi.

Katika kufikia azma ya kiuchumi, Tanzania na Uganda zimeingia mkataba wa awali wa makubaliano  ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ukiwemo ule wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), utakaogharimu Sh8 trilioni kutoka Kabaale - Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania.

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni Makamu wa Rais wa Burundi,  Prosper Bazombanza Wawakilishi kutoka Jumuiya ya Falme za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Peter Mathuki, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Uganda, mawaziri, wabunge na wananchi.