Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC awatangazia kiama wauza pombe

Muktasari:

Nkurlu alisema vijana wengi badala ya kufanya kazi wanakimbilia kunywa pombe na kuvuta dawa za kulevya.

Kahama. Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu amewatangazia kiama wauza pombe wakati wa kazi akisema  ataanzisha msako wa nguvu kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Nkurlu alisema vijana wengi badala ya kufanya kazi wanakimbilia kunywa pombe na kuvuta dawa za kulevya.

Wakati Nkurlu akipiga marufuku kitendo hicho, Umoja wa Wamiliki wa Baa na Nyumba za Kulala Wageni wilayani Kahama, umeunga mkono agizo la kufungua baa saa kumi jioni siku za kazi.

Mwenyekiti wa umoja huo, Julias Machage alisema agizo hilo ni la kitaifa na wanalikubali. 

 Machage alisema wamepokea barua kutoka Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ikiwataka kufunga baa wakati wa kazi.

Nkurlu alisema atawachukulia hatua wafanyabiashara watakaokutwa wanafanya biashara hiyo muda wa kazi.