Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chongolo: Suala la bandari ni la CCM, sio la mtu binafsi

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa CCM, Daniael Chongolo amesema suala la mkataba wa bandari ni la chama hicho na siyo la mtu mmoja na kuiagiza Serikali kuharakisha mchakato kwenda kwenye uwekezaji.

Iringa. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka Watanzania wasikubali kupotoshwa kuhusu mkataba wa uwekezaji bandarini kwa sababu utakuwa na manufaa mengi ta Taifa.

 Amesema mkataba huo ni wa CCM sio mtu mmoja na amesisitiza kuwa suala hilo lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020, ibara ya 59 na ukurasa wa 92 kuhusu uboreshaji wa bandari.

Chongolo amesema hayo leo Julai 15, 2026 wakati akihutibia wananchi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Ruanda Nzovwe, jijini Mbeya.

Amesema kuna watu wametengeneza uongo ili kusapoti dhamira ya kupotosha uboreshaji wa bandari nchini.

“Serikali imepewa msukumo na chama kinasimamia kuhakikisha utekelezaji unafanyika, naagiza Serikali ichakate haraka kuelekea kwenye mkataba wa uwekezaji wa bandari,” amesema Chongolo na kuongeza.

“Kazi ya maneno ya siasa ni ya wanasiasa, watendaji wasihangaike kujibu. Eti jambo la fulani hata angekuwa nani ndani ya CCM, agenda isiyo na maslahi ya watu haitapita.”

Amesema ilani hiyo ya CCM ndiyo iliyoweka ahadi ya kuboresha bandari zote nchini.

“Aliyeandaa ilani ndiye aliyeweka haya malengo, mjadala wa ilani ulianza mwaka 2020. Tuliahidi, baada kuahidi tunatekeleza. Tukicheka na wanaopotosha adhabu itakuwa kwetu,” amesema Chongolo.

Amesema CCM itakusanya maoni ya wananchi na yale yenye tija yatafanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa Chongolo, takwimu zinaonyesha kuwa bandari kwa sasa inaingiza zaidi ya Sh7 trilioni huku asilimia 99 ya fedha hizo ikitumika kwa matumizi yao wenyewe.

“Nani anakula hizo Sh7 trilioni? Sasa wakiambiwa ulaji unakatwa watafunga midomo? Kuna genge la watu wana mlo na hawataki kuona mambo yanabadilika,” amesema na kuongeza;

“CCM tuna akili timamu na habari yao wataipata, tija ikipatikana. Msikubali, msiyumbishwe agenda ni ya CCM sio ya mtu.”

Chongolo amesema hawezi kusimama na kutetea jambo ambalo haoni tija kwa Watanzania.

Amesema ikiwa kuna mwana CCM hajasimama kupigania suala hilo lazima kuna mashaka na uana-CCM wake na sio vinginevyo.

“Ukiona adui yako anakupigia makofi unapotaka kufanya jambo achana nalo, hatufungi breki na niagize Serikali ichakate haraka tusonge mbele,” amesema.