Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbarawa ataja sababu za Serikali kuichagua DP World

Waziri wa Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa.

Muktasari:

  • Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amezitaja sababu za Serikali kuamua kuichagua Kampuni ya DP World katika kufanya shughuli za uboreshaji wa bandari hapa nchini.

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa amezitaja sababu za Serikali kuamua kuichagua Kampuni ya DP World katika kufanya shughuli za uboreshaji wa bandari hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano na Wahariri leo jijini hapa, Prof Mbarawa amesema DP World ina uwezo mkubwa katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini, na Australia.

“DP World ina uwezo na utaalamu wa kuchagiza katika mmonyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambayo bidhaa zinatoka mpaka kwa walaji wa bidhaa hizo,” amesema Prof mbarawa.

Pia ameongeza kuwa sababu nyingine ni kampuni hiyo kumiliki meli zaidi ya 400 za mizigo kupitia kampuni yake nyingine, jambo ambalo litaongeza ufanisi mkubwa katika usafirishaji wa mizigo.

Aidha amesema kampuni nyingine hazikukidhi sifa za mwekezaji mahiri ambaye anahitajika kwa bandari ya Dar es Salaam kwa sababu hazikuwa na uwezo wa uchagizaji wa mnyororo mzima wa usafirishaji wa mizigo.