Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msimamo wa Yanga ishu ya dabi, yaigomea CAS

Muktasari:

  • Kanuni ya 27 (i) ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu inafafanua kuwa vyombo vya maamuzi vya TFF na TPLB vitashughulikia masuala na mashauri mbalimbali kuhusiana na Ligi Kuu na kufanya maamuzi kwa misingi ya kanuni na mwongozo wa katiba ya TFF.

Dar es Salaam. Licha ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuamuru Yanga kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za TFF kushughulikia malalamiko yao, klabu hiyo imeendelea kushikilia msimamo wake wa kutocheza meche ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Simba.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumatatu Mei 5, 2025 na Kamati ya Utendaji ya Yanga, imesema imepokea majibu ya kesi namba CAS 2025/A/11298 na kuelekezwa kufuata utaratibu wa ndani kabla ya kufikia hatua ya rufaa.

Hata hivyo, uongozi wa Yanga umekataa maagizo hayo ukieleza kutokuwa na imani na mamlaka za soka nchini, wakidai kuna "uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa wazi kwa baadhi ya timu."

Kutokana na msimamo huo, Yanga imetangaza rasmi kuwa haitashiriki mchezo wake wa mzunguko wa pili dhidi ya Simba SC, ambao ni wa 184 wa Ligi Kuu Bara msimu huu, wakisema hawako tayari kushiriki mchuano huo kwa namna yoyote ile.

"Msimamo wa klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko pale pale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imehitimishwa kwa kuwataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa tayari kupambana kwa njia zote kuhakikisha haki inapatikana na kulaani kile walichokiita "dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kanuni unaofanywa na mamlaka za soka."

Mei Mosi mwaka huu, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ilitoa taarifa ya kufuta na kutoendelea na shauri lililofunguliwa na Yanga kuhusu mchezo wake wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ulioahirishwa dhidi ya Simba, Machi 8, 2025.

Yanga iliiomba CAS mechi ya marudiano ya Ligi Kuu baina yao na Simba isipangiwe tarehe na pia ipewe pointi za mezani.

Mechi hiyo ilikuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu lakini ikaahirishwa baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, siku moja kabla ya mchezo.

CAS iliamua kutupilia mbali shauri hilo kwa vile Yanga haikufuata utaratibu wa kushughulikia malalamiko yake kwa kupeleka shauri hilo CAS kabla ya kuanza na vyombo vya ndani.

CAS iliiagiza Yanga kupeleka shauri hilo kwanza katika mamlaka za ndani za uendeshaji soka na baada ya hapo ndio ilifikishe katika mahakama hiyo.