Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bunge laanza kuifanyia kazi ripoti ya escrow

Wabunge wakiendelea na kikao cha Bunge Dodoma.Picha na maktaba

Muktasari:

Ni baada ya kuwasilishwa na CAG bungeni sasa kujadiliwa na Bunge Novemba 26 mwaka huu

Dodoma. Ripoti ya kashfa ya fedha zilizochotwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow kutoka Benki Kuu (BoT), imejadiliwa jana katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge.

Habari zilizopatikana kutoka ndani na kikao hicho na kuthibitishwa na Naibu Spika Job Ndugai, zinaeleza kuwa suala hilo lilijadiliwa na litawasilishwa bungeni Novemba 26.

Kwa mujibu wa habari hizo, ripoti imekabidhiwa kwa Katibu wa Bunge ili yeye na wataalamu wake waipitie na kuikabidhi kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikal i(PAC), kwa ajili ya kuiwasilisha bungeni.

Ndugai

Naibu Spika, Job Ndugai alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema limejadiliwa na kwamba ratiba iko vilevile katika kuwasilishwa kwake.

Alisema taarifa kamili ya kikao hicho ataiwasilisha bungeni katika kikao cha Jumatatu.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa ripoti hiyo inaweza kuondoka na vigogo serikalini waliohusika kuchota fedha hizo.

Baadhi ya wenyeviti wa kamati waliohudhuria kikao cha kamati ya uongozi jana waligoma kuzungumzia kilichojiri, wakieleza kuwa suala hilo lipo kama lilivyopangwa.

Suala la ufisadi huo liliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila na kwamba linawahusisha vigogo wa ngazi za juu serikalini.

Ufisadi huo wa Sh200 bilioni katika akaunti hiyo, umekuwa gunzo katika mkutano wa Bunge unaoendelea kiasi cha suala kuuliziwa kila siku na wabunge

Hivi karibuni Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje alidai kuwa kutokana na uzito wa ufisadi huo, wamesikia kwamba kuna naibu waziri mmoja mdogo anaandaliwa kisaikolojia ili aweze kutolewa kafara.

Hata hivyo, Wenje hakumtaja waziri huyo huku akisisitiza kuwa ripoti hiyo lazima iondoke na mtu.

Inaelezwa kuwa serikali imekuwa ikihaha kuhakikisha mambo yanakaa sawa, lakini baadhi ya wabunge wanasema hawatakubali ripoti hiyo ichakachuliwe hivyo ni lazima ing’oke na mtu.

Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa wangependa suala hilo liwe wazi na kwamba Bunge lingeruhusu kila kitu kiwe wazi ili kuondoa minong’ono inayoendelea chini chini.

Hata hivyo, Bunge limekuwa likishikilia msimamo wake kwamba ripoti hiyo itawasilishwa kama ilivyopangwa na wabunge watakabidhiwa nakala zake.

Akaunti ya Escrow

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa baada ya kutokea mgogoro kati ya Kampuni ya IPTL na Tanesco. Ilifunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Sakata hilo limechukua sura mpya baada ya PAC, kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwasilisha taarifa ya uchunguzi wa akaunti hiyo mbele ya kamati hiyo ifikapo Oktoba 31, mwaka huu.

Hata hivyo, katika taarifa yake hivi karibuni, ofisi ya CAG ilisema: “Ukaguzi wa Akaunti ya Tegeta Escrow uliombwa na Katibu wa Bunge na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini na unalenga kufanya uchunguzi wa kina utakaotoa taarifa kamili yenye kuonyesha hali halisi kuhusu akaunti maalumu ya Tegeta.