Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Biteko aagiza wadau wa utalii kubuni mazao mapya ya utalii

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko akikagua baadhi ya mabanda katika maonyesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu Kilifair, leo Ijumaa Juni 6, 2025 katika Viwanja vya Magereza (Kisongo)

Muktasari:

  • Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema ni muhimu Wizara na wadau wa utalii kushirikiana na kubuni mazao mapya ya utalii ili kukuza sekta hiyo.

Arusha. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ameagiza Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na wadau wa utalii nchini, kubuni mazao mapya ya utalii na kutumia teknolojia ya kisasa ili kuongeza chachu kwenye sekta hiyo na kuweza kushindana kimataifa.

Dk Biteko ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Juni 6, 2025 wakati akifungua Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu Kilifair yaliyofanyika katika viwanja vya Magereza (Kisongo) mkoani Arusha.

Amesema ni muhimu kuanzisha mazao mapya ya utalii na Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inatumia Tehama katika kutangaza utalii na upatikanaji wa masoko ya utalii na kishirikiana na wadau mbalimbali ili kuboresha mazingira ya biashara za utalii nchini ili kuchochea na kuvutia uwekezaji zaidi.

"Nitumie fursa hii kuielekeza wizara kutekeleza mambo machache ikiwemo kuendelea kubuni njia mbalimbali za uendelezaji wa mazao ya utalii nchini kwa kuzingatia mgawanyo wa aina ya mazao," amesema.

"Mtawanyiko wa kijiografia maana yake ni kwamba kuna mahali kuna zao la aina fulani la utalii aidha ni wanyama, malikale au vivutio vingine vya asili vilivyopo basi wizara iangalie mtawanyiko huo na kuutafutia ubunifu wake ili uweze kuwa na manufaa na kuongeza mchango kwenye utalii," amesema.

Amesema Tanzania kwa mwaka 2024 imeweka rekodi ya kufikia watalii 5,360,247, huku sekta ya utalii ikiingiza mapato ya Dola za Marekani 3.9bilioni na kuendelea kuzalisha fursa mbalimbali za ajira na uwekezaji.

Sekta ya utalii imeendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuhifadhi maliasili na malikale, ustawi wajamii na ukuaji wa uchumi ambapo takwimu zinaonyesha kuwa sekta ya utlii inachangia asilimia 17 ya pato la taifa, asilimia 25 ya mauzo yote ya nje ya nchi kwahiyo sekta hii ni muhimu katika kutuletea fedha za kigeni kwaajili ya uchumi wa nchi yetu," ameeleza.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amesema kuwa Sera ya taifa ya utalii imetilia mkazo imetilia mkazo suala la kukuza utalii endelevu ambalo moja ya misingi yake ni ushirikiano wa wadau na wa sekta ya umma na binafsi katika kuendelea kutangaza utalii nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa si chachu ya mafanikio bali mwezeshaji na mtengenezaji wa uchumi imara unaonufaisha wananchi.

"Tunatekeleza ilani ya CCM ndoto iliwekwa kuhakikisha sekta ya utalii inakua, haya yanayoonekana hapa ni ushirikiano wa wadau wote ikiwemo sekta binafsi na eneo hili la maonyesho ni eneo la Magereza ila leo tumeomba leo Magereza watupe eneo hili liwe la kudumu la maonyesho haya ili tuliboreshe zaidi kwa ajili ya maonyesho," amesema.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amepongeza maonyesho hayo na kuwa yamekuwa chachu ya sekta ya utalii.

"Nimekuja kuona maonesho haya ya utalii yanayohusisha nchi zaidi ya 50, Rais wetu alipoingia akafanya filamu ya Royal Tour, watekelezaji ni kama Mkuu wa Mkoa, Rais ameonyesha njia, hapa unaonyesha kwa vitendo kila kukicha matukio makubwa yanayochochea utalii mkoa wa Arusha ni wazi watalii wameongezeka mapato yanaongezeka na yote haya yanakwenda kuchangia mapato ya serikali," amesema.

"Kwenye suala la utalii nikupongeze sana unamuwakilisha Rais kwenye utalii, kuhakikisha kwa sababu ya utalii suala la amanii na utulivu na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo naomba na mikoa mingine waige maonyesho haya ili kukuza uchumi wetu," amesema.