Baba adaiwa kumuua mwanaye

Muktasari:
- Jeshi la polisi mkoani kilimanjaro linamshikilia mkazi wa kijiji cha Challa wilayani Rombo, John Kavishe (77) kwa tuhuma za kumuua mwanaye, Amedeus (31) kwa kumkata na panga shingoni wakati akisuluhisha ugomvi wa kifamilia.
Rombo. Jeshi la polisi mkoani kilimanjaro linamshikilia mkazi wa kijiji cha Challa wilayani Rombo, John Kavishe (77) kwa tuhuma za kumuua mwanaye, Amedeus (31) kwa kumkata na panga shingoni wakati akisuluhisha ugomvi wa kifamilia.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea Julai 10, 2021.
"Marehemu alikuwa na ugomvi na mke wake ndipo baba mzazi alipokwenda kusuluhisha kitendo hicho kilimchukiza marehemu akaanza kumtukana baba yake ambaye alipandwa na hasira na kuchukua panga na kumkata mwanaye shingoni," amesema Kamanda Maigwa.
Amebainisha kuwa mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Ngoyoni kilichopo wilayani Rombo.