Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ate yahimiza waajiri kupitia mchakato tuzo za muajiri bora

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (Ate), Suzanne Ndomba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mchakato wa tuzo ya muajiri bora kwa mwaka 2023, katika ofisi za Chama hicho zilizopo jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Chama cha Waajiri Tanzania ATE, leo kimezindua mchakato wa utoaji tuzo kwa waajiri bora ikiwa ni sehemu ya kuongeza ubora wa mazingira mazuri ya kazi.

Dar es Salaam. Katika juhudi za kuongeza chachu kwa waajiri kuwa na mazingira bora ya utendaji na ushindani, Chama Cha Waajiri nchini (Ate), leo kimezindua rasmi mchakato wa kutafuta muajiri bora kwa mwaka 2023.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti maalumu ya mchakato huo makao makuu ya Ate jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Suzanne Ndomba amesema lengo la tuzo hiyo ni kuwatambua waajiri wanaofanya vizuri kwa kuzingatia usimamizi wa rasilimali watu.

"Tuzo hii imeanzishwa mwaka 2005 imeendelea kuwa muhimu kwakuwa dhumuni lake linatambua waajiri wanaofanya vyema katika kuweka mikakati bora ili kuongeza tija katika biashara," amesema Ndomba.

Amesema tuzo hizi zimehamaisha waajiri kuweka sera bora za ajira na kuweka mahusiano bora mahala pa kazi utii wa sheria na ushindani.

"Kama mnakumbuka mwaka jana mwishoni tulitoa tuzo, lakini Mei mwaka huu tumefanya mkutano na wale walioshiriki kwa ajili ya kuwapa mrejesho na kupata maoni yao ili nasisi kama Ate tuweze kuboresha tuzo hizi," amesema.

Ndomba amesema suala hili linawaweka waajiri katika namna ya kuvutia kwasababu anapochukua tuzo anakuwa na uhakika wa mazingira bora kwa wafanyakazi wake.

Mwisho amewataka wanaotaka kushiriki waendelee kujitokeza ili kuanza mchakato huo ambao una vipengele 14, vikiwemo vihusuvyo usawa wa kijinsia, ubora katika usimamizi wa rasilimali watu, utawala na uongozi, ushirikishwaji wa muajiriwa, mabadiliko ya tabianchi, na namna ambavyo kampuni zinakabiriana na majanga kama Uviko-19.