Askofu Romwa astaafu, Kilaini Mwangalizi wa Kitume Bukoba

Muktasari:
- Baba Mtakatifu Francisco amekubali ombi la Askofu wa Jimbo la Bukoba, Desederius Romwa kustaafu baada ya kufikisha umri wa miaka 75.
Dar es Salaam. Baba Mtakatifu Francisco amekubali ombi la Askofu wa Jimbo la Bukoba, Desederius Romwa kustaafu baada ya kufikisha umri wa miaka 75.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Oktoba Mosi, 2022 na Katibu Mkuu TEC, Charles Kitima imeeleza kuwa Askofu Desderius Romwa anastaafu rasmi leo.
“Baba Mtakatifu anamshkuru na kumpongeza Askofu Desiderius Romwa kwa uchungaji uliotukuka Jimboni Bukoba,” imeeleza taarifa hiyo.
Wakati huo huo Baba Mtakatifu amemteua Askofu Methodius Kilaini kuwa Mwangalizi wa Kitume wa Jimbo la Bukoba kwa kipindi hiki Jimbo hilo linaposubiri kupata Askofu.
Uteuzi huo unaanza leo Oktoba Mosi 2022.
Mpaka sasa Askofu Methodius Kilaini ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba.