Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lori laparamia nyumba na kuungua, wanne wajeruhiwa

Muktasari:

  • Dereva wa lori lililosababisha ajali amekimbia.

Dar es Salaam. Watu wanne wamejeruhiwa baada ya lori lililobeba saruji kuacha njia, kugonga maduka sita na nyumba moja pembezoni mwa barabara ya Wazo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Majeruhi hao, Ezekiel Matuni, Herubu Jackson na Stanley Mchingwi na mmoja ambaye hajatambuliwa jina, wamefikishwa katika Hospitali ya Kitengule.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 10, 2025 Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Kinondoni, Jacob Chacha amesema ajali hiyo imetokea saa 3:50 asubuhi ya leo.

Amesema lori hilo lilikuwa likitokea kiwanda cha saruji cha Wazo kuelekea Tegeta na lilipata hitilafu ya mfumo wa breki likiwa kwenye mteremko.

"Jumla ya fremu ambazo zimeparamiwa zilikuwa sita lakini pia nyuma yake kulikuwa na nyumba ambayo vyumba viwili vimeathirika kutokana na ajali hiyo," amesema.

Kamanda Chacha amesema dereva amekimbia baada ya ajali iliyosababisha moto eneo la kichwa cha lori.