Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Gwajima: Nitakwenda kamati ya Bunge kusema ukweli

Askofu Gwajima: Nitakwenda kamati ya Bunge kusema ukweli

Muktasari:

  • Mbunge wa Kawe na Askofu wa Kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekiri kupokea barua ya wito wa kuitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mbunge wa Kawe na Askofu wa Kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekiri kupokea barua ya wito wa kuitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Jana, ilisambaa mitandaoni barua ya ofisi ya Bunge ikionyesha Gwajima na mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa wanatakiwa kwenda mbele ya kamati hiyo Agosti 23 na 24.

“Nimepokea barua ya Spika kwenda kwenye kamati, nitakwenda. Nimesema hapa kwa kuwa aliyenitumia barua ameweka mitandaoni akisema kwanini nimesema hapa na yeye aniambie kwa nini aliweka mitandaoni,” amesema Gwajima leo, Agosti 22, 2021 alipokuwa akizungumza na waumini wake katika kanisa hilo, Dare es Salaam.

Askofu Gwajima amesema atakwenda kwenye kamati hiyo na atasimamia ukweli kama ambavyo imani yake inamtuma.

 “Nitakwenda kwenye kamati wategemee ukweli nitasema ukweli kwa kuwa imani ya CCM ni ukweli na nitaongeza mengine ambayo sijawahi kusema. Lazima tusimamie nchi na watoto wa watoto wetu,” amesema askofu Gwajima.