Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua viongozi wanne

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan ameteua wenyeviti wanne wa bodi wa mashirika mbalimbali ya Serikali.

Dodoma. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameendelea kuimarisha taasisi za umma kwa kufanya uteuzi wa viongozi wanne wa mashirika ya Serikali.

Tarifa iliyotolewa leo Jumanne, Aprili 29, 2025 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka imebainisha walioteuliwa ni wenyeviti wa bodi.

Rais Samia amemteuwa Dk Fatma Kassim Mohamed kuendelea na wadhifa wake kama Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa kipindi cha pili mfululizo.

Pili, Dk Jilly Maleko ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), akichukua nafasi ya Balozi Begum Karim Taj ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.

Pia, Rais Samia amemteua Profesa Eliakimu Zahabu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon Monitoring Center - NCMC), taasisi inayohusika na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Lucas Mwino, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), akichukua nafasi ya Dk John Mduma aliyemaliza muda wake," taarifa hiyo inaeleza.