Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumlawiti mtoto

Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Geita

Muktasari:

  • Kesi hiyo namba 18958 imesomwa leo Julai 12, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Nyakato Bugirwa.

Geita. Mkazi wa Kijiji cha Bugogo kilichopo Wilaya ya Geita mkoani Geita, Rwaketa Herman (30), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.

Kesi hiyo namba 18958 imesomwa leo Julai 12, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Nyakato Bugirwa.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Deodatha Dotto ameieleza Mahakama kuwa Juni 14, 2024 huko Bugogo wilayani Geita, mshtakiwa alimuingilia kinyume na maumbile mtoto huyo (jina linahifadhiwa).

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amepelekwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili na mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh2 milioni.

Wakati huohuo, Emanuel Karim (19), mkazi wa Nyamatagata wilayani Geita, amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 13.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Deodatha Dotto ameieleza Mahakama kuwa Juni 9, 2024  huko Nyamatagata wilayani Geita, mshtakiwa alimuingilia kinyume na maumbile mtoto mwenye jinsi ya kiume.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa na amerudishwa mahabusu baada ya kushindwa masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili na mali isiyo hamishika yenye thamani ya Sh2 milioni.

Kesi hizo zimeahirishwa hadi Julai 22, 2024 zitakapokuja kwa ajili ya kutajwa.