Angalia hapa matokeo darasa la saba 2022...

Muktasari:

Necta imetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ukionyesha asilimia 79.62 wamefaulu katika madaraja ya A, B na C.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu likisema watahiniwa zaidi ya 1.07 milioni kati ya 1.34 milioni wenye matokeo sawa na asilimia 79.62 wamefaulu kwa kupata madaraja A na B na C.



Kati ya hao wasichana ni 558,825 ambao ni sawa na asilimia 78.91 na wavulana ni 514,577 sawa na asilikia 80.41.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi ametangaza matokeo hayo leo Alhamisi Desemba Mosi, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini hapa kuhusu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.

Almasi amesema katika matokeo ya mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 907,802 sawa na asilimia 81.97.

Amesema kitakwimu kuna kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka jana.