Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKU yanoa walimu wa msingi, sekondari kufundisha STEM kwa njia shirikishi

Walimu kutoa shule mbalimbali za msingi na sekondari wakifuatilia mafunzo ya namna ya kufundisha masomo ya STEM kutumia teknolojia. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chuo Kikuu cha Agan jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU) kimeendelea kuhimiza maendeleo ya masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) kwa kutoa mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari, kutoka shule za Serikali na binafsi.

Hayo yamesemwa jana Aprili 28, 2025 na Amidi wa AKU, Dk Jane Rarieya kwenye taarifa ya ufunguzi wa warsha iliyohusu kuwajengea uwezo walimu kuhusu masomo ya STEM iliofanyika chuoni hapo, jijini Dar es Salaam.

Dk Jane Rarieya amesema lengo la mpango huu ni kuwafikia moja kwa moja walimu na wanafunzi walioko shuleni, ili kuboresha uelewa na ufundishaji wa masomo hayo muhimu.

"Ni dhamira ya AKU kuhakikisha walimu na wanafunzi wanashiriki kikamilifu katika ujifunzaji unaomuhusisha mwanafunzi kwa vitendo zaidi," amesema Dk Rarieya.

Amesema mafunzo hayo yanawapa walimu mbinu mbalimbali za kufundishia kupitia teknolojia ambazo zinamuwezesha mwanafunzi kujifunza kwa kutenda.

"Walimu wamefundishwa ujuzi mbalimbali unaosaidia kuibua maarifa kwa wanafunzi endapo mbinu bora zitatumika.

"Kwa sasa, nyenzo zilizotumika katika mafunzo hayo hazihusishi tu somo la fizikia bali pia zimepanuliwa kuhusisha masomo ya kemia, biolojia, hisabati na jiografia," amesema Dk Rarieya.

Amesema mbinu hizo mpya zinalenga kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni, hasa kwa masomo ambayo mara nyingi yamekuwa magumu kwa walimu na wanafunzi kuyamudu.

Dk Ester Kibga ambaye ni mkufunzi na mwezeshaji wa mafunzo hayo, amesema  yamepata mwitikio mkubwa kutoka kwa walimu wa ngazi na taasisi mbalimbali, jambo linaloonyesha uelewa mpana kuhusu umuhimu wa masomo ya STEM.

“Masomo ya STEM hayafundishwi kama mengine mashuleni. Huko shuleni tunafundisha sayansi, kemia, fizikia, historia, biolojia na hisabati.

"Kupitia mafunzo haya, tunataka walimu waone umuhimu wa kuwafundisha watoto vizuri masomo haya kwa sababu ni ya msingi sana katika zama hizi za maendeleo ya teknolojia," amesema Dk Kibga.

Ameria Kianga kutoka Benki ya DTB ambao ni wadhamini wa mafunzo hayo amesema  benki hiyo imevutiwa na mafunzo hayo kwa kutoa msaada wa elimu ya kidijitali kwa walimu na wadau mbalimbali wa elimu.

"Kupitia mafunzo haya, tumetambua nafasi ya kuwaelimisha walimu kuhusu huduma zetu, ikiwemo utoaji wa mikopo bila kujaza fomu na kuwasaidia kuanzisha akaunti za watoto ili kuweka akiba kwa ajili ya malengo ya baadaye," amesema Ameria.

Mwezeshaji wa mafunzo kutoka AKU iliyopo Mombasa nchini Kenya, Charles Muigai, amesema amevutiwa na mtindo wa mafunzo kwa vitendo, unaowawezesha walimu kuelewa na kufundisha kwa ufanisi zaidi.

"Kwa kutumia “Physics Education in Technology” (PhET), nimeweza kupata ujuzi wa kuwaonesha walimu mambo kwa vitendo kwa ujasiri zaidi.

Mugai amesema matarajio yake ni kuwaelimisha zaidi walimu anaowafundisha, ili nao waweze kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.